Mheshimiwa mkuu wa wilaya Julius Mtatiro leo tarehe 13 januari 2023 amegawa vishikwambi kwa walimu katika wilaya ya Tunduru kutimiza agizo la raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr samia suluhu hassani la kuwagawia vishikwambi walimi wote Tanzania ili kuboresha utendaji kazi katika sekta ya elimu.
walimu 1,448 ambayo ni idadi ya walimu waliopo katika wilaya ya Tunduru walitarajiwa kupata vishikwambi ivyo , idadi ya vishikwambi vilivyopo katika wilaya ya Tunduru ni 1,405 ambavyo vimepokelewa toka TAMISEMI , vishikwambi hivyo vimegawiwa kwa walimu 1,015 wa shule za msingi zilizopo Tunduru na vishikwambi 422 vimegawiwa kwa walimu wa shule za sekondari zilizopo Tunduru na kufanya upungufu wa vishikwambi 43 kutimiza idadi yote ya walimu waliopo katika wilaya Ya Tunduru.
Mkuu wa wilaya alimshukukru raisi Dr Samia suluhu hassani kwa kutimiza ahadi yake hiyo ya kuwagawia vishikwambi walimu wote katika wilaya ya Tunduru na Tanzania nzima na kuwataka walimu hao kutumia vishikwambi hivyo kwa maslahi mapana ya kuboreshe sekta ya elimu ili kuwa na elimu bora kwa wanafunzi wa Tanzania.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.