Mh. Mkuu wa wilaya ya Tunduru Ndg Julius Mtatiro afanya ziara katika kijiji cha milonde, kata ya Matemanga, tarafa ya Matemanga , wilaya ya Tunduru , inayohusu kusikiliza kero za wananchi na kuwapa nafasi Ya kutoa (kueleza) kero zao.
Ndg Said Said mkazi wa kijiji cha milonde alitoa malalamiko kuhusiana na kutokamilika kwa mradi wa maji ambao unakadiliwa kuwa na zaidi ya miaka mitano (5) na kuiomba serikali kuwasaidia kuhusiana na suala ilo.
Ndg Mohamedi Omary Mkonga mkazi wa kijiji cha milonde aiomba halmashauri ya wilaya ya Tunduru iweze kuongeza shule ya msingi katika kijiji icho kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ambao wengine wanashindwa kuendelea na masomo na kusababisha kurudia darasa moja kwa mda wa miaka mitatu.
Mh. Mkuu wa wilaya ya Tunduru alitoa baadhi ya majibu kuhusiana na malalamiko(kero) za wananchi wa kijiji cha milonde, alitoa maagizo kwa gavana na diwani kukaa kikao na wananchi kujadili suala la ujenzi wa shule, na kupitia suala la maji aliacha maagizo kwa mwenyekiti wa kijiji apange tarehe ya kukutana na RUWASA ili kujadili ilo suala la maji.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.