Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) chini ya Wizara ya Maliasili naUtalii wanaendelea kujikita juu ya kutataua Migongano ya Shughuri za kibinadamu na Wanyama Pori waaribifu hususani Tembo.
JET ilikita kambi katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuweza kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma na Lindi juu ya kuweza kupambanua Habari za mgongano baina ya wanyama Pori na Shughuri za Kibinadamu.
Katika Mafunzo hayo ambayo walihudhuria wawakilishi kutoka Shirika Ujerumani GIZ walielezea kuwa kuna jitihada mbalimbali wamezifanya kwaajili ya kuweza kunusuru maisha na mali za wananchi katika maeno mbali mbali katika vijiji vilivyo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Chama hicho chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake mkuu Bw.John Chikomo kilipata Fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo ambayo Kuna migongano na miingiliano baina ya shughuri za kibinadamu na wanyama pori waaribifu na kupata nafasi ya kusikiliza changamoto zinazo jitokeza katika maeneo yao kutoka katika uongozi wa Serikali ya kijiji na wananchi wameneo husika kama vile Kijiji cha, Machemba,Mbati,Mbesa,na Ngapa.
Aidha, JET kilitoa pongezi dhidi ya Shirika la GIZ kwa mbinu mbalimbali walizo zifanya kwa wananchi kuweza kuwadhibiti wanyamapori Tembo kwa kuzungushia uzio wa pilipili katika mashamba ya pamoja ya vijiji,Kuwapeleka mafunzo Vijana wa VGS Village Game Scout nakuweza kusaidia katika maeneo yao yanayo wazunguka.
Pia, Uongozi wa JET pamoja na waandishi wa habari kutoka katika vyanzo mbalimbali walipata fursa ya kukutana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndugu Bosco Oja Mwingira na aliweza kutoa ufafanuzi juu ya jitihada zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru dhidi ya kutatua migongano hiyo.
Imetolewa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,
Orpa Kijanda,
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.