Kampuni ya Carbon Tanzania imedhamiria kuja kuwekeza Halmashauri ya Wilaya Tunduru kampuni hiyo uwekeza kwa kuifadhi mazingira na sio kuharibu mazingira yanayo tuzunguka hayo yamesemwa na Bw.Mack Bakari ambae ni Mkurugenzi Wa Carbon Tanzania.
Amesema lengo la kufika Tunduru na Kuonana na Uongozi wa Wilaya lengo kupata Baraka za viongozi hao wa wilaya pia malengo ya Kampuni ni kuwekeza katika kuvuna hewa ya carbon inayopatikana kwenyenye miti ya asili.
Aidha baada ya kuvuna hewa hiyo itauzwa kwenye soko la kimataifa kasha gawio litarudishw kwenye vijiji husika vilivyo tunza msitu nikama faida ya sehemu ya kutunza misitu hiyo aidha amewataka wananchi wa Tunduru waupokee mradi huo ni mzuri na unahamasisha Wananchi Kutunza Mazingira ili yatutunze.
Kwa Upande wa Dc Mtatiro aliwomba Waheshimiwa Madiwani wakawe mabalozi wazuri kwa Wananchi kuhusu mradi huo wa Kaboni Tanzania maana unakuja kubadilisha maisha ya Wananchi wetu zaidi uchumi wa vijiji ambavyo vina misitu mikubwa lakini hawajui watumiaje misitu yao.
Dc Mtatiro alisema kampuni ya Carbon Tanzania yenyewe haikati miti bali ufanya kazi yake ya kuhamasisha Wananchi wa kijijihusika watunze Misitu na mazingira yanayo wazunguka kwa ujumla lengo mwisho wa mwaka kampuni hiyo ya Carbon Tanzania itakuja na vifaa vyake vya kisasa kupima kiwango cha hewa ya Carbon iliyopo katika msitu huo kisha uchukua takwimu hiyo na kuipeleka katika soko la kimataifa na kuiuza kisha kiwango cha pesa kitakacho patikana gawio 60% litarudishwa kijijini kwajili ya Wananchi wahamue nini fanye katika kijiji chao.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Tunduru Bw. Chiza Marando aliwaomba wawekezaji wa Carbon Tanzania katika 10% ya Halmashauri waongeze kidogo adi 20% lengo kuiwezesha halmashauri iweze kuhudumia Wananchi kwa wakati kwa upande wake Bw. Bakari Mkurugenzi wa Carbon Tanzania alikubali ombi hilo alisema kampuni yake ya Carbon Tanzania imelipokea ombi hilo na litafanyiwa kazi wakati ukifika alisema.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.