Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh Juma Homera wakati akitoa salamu za serikali katika mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa klasta wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Aidha aliendelea kusema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imechuguliwa na bodi ya korosho kama sehemu ambayo watajenga ghala la kisasa la kuhifadhia korosho na mpaka sasa taratibu za ujenzi zinaendelea kwa kusafisha eneo la ekari kumi tayari kuanza ujenzi huo mara moja.
Aidha Mh Homera alisema kuwa pembejeo za korosho mwaka huu zitatolewa bure kwa wakulima ambao watapalilia mikorosho hivyo kuwataka wananchi kufanya palizi katika mashamaba ya mikorosho.
Vilevile alitaka haki kutendaka katika ugawaji wa pembejeo za korosho ili kuondoa malalamiko kwa wananchi, na kusisitiza kuwa viongozi wa vijiji na kata kusimamia kwa karibu ila kila mkulima wa korosho ajiandikisha mapema.
Hata hivyo Mh Homera aliwataka wahesimiwa madiwani kutumia kamati ya maendeleo ya kata kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo, vyanzo vya mapato, ujenzi wa matundu ya vyoo, madarasa ili kuboresha miundombinu katika maeneo yao ya uongozi.
“tumieni mabaraza ya kata kuibua miradi ya maendeleo, pangeni mkakati wa kupunguza matatizo ya katika shule kama ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na matundu ya vyoo”
Vile vile alikumbushia suala la ukusanyaji wa mapato kusimamiwa na kufuatiliwa kwa weledi hasa katika maeneo ya stand na sokoni, kwani kuna baadhi ya magari ya kwenda vijiji yanapaki nje ya standi ili kukwepa kulipa ushuru.
“Niwaombe Halmashauri hasa idara inayosimamia mapato kuangalia kwa ukaribu watu wanaokwepa ushuru na kutenga eneo kwa ajili ya kupaki magari madogo ili kuweza kukusanya mapato yanayopotea” alisema Mh Homera.
Sambamba na hayo aliwataka madiwani kushirikiana na wataalam katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayopelekwa katika Kata zao na pia kamati ya fedha kukosoa dosari zinazoonekana katika miradi ya maendeleo.
“serikali haitakaa kimya kwa mtendaji yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake na itawashughulikia Wakuu wa Idara atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa Umma” alisema mkuu wa wilaya.
Aliendelea kusemakuwa kuna udanganyifu unaofanywa na vyama vya msingi kwa kutotumia kibali cha ununuzi wa mazao kutoka Halmashauri, na baadhi yao wanasafirisha mazao kwa kutumia mabasi hivyo kuwataka waache mara moja.
Homera alisema kuna chama cha msingi cha SAM waliosafirisha mbaazi gunia 20 kupitia basi na kumuomba Afisa Ushirika Wilaya kuwachukutulia hatua za haraka na kukifuta chama hicho cha msingi mara moja kwa kukiuka sheria za ushirika.
Theresia mallya.
Afisa Habari (w)
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.