Tunduru 26/02/2020
Hayo yamesemwa na mratibu wa mradi wa kunusuru kaya maskini wilayani Tunduru wakati wa malipo ya kipindi cha mwezi Machi na April 2019 yanayofanyika baada ya uzinduzi wa utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini (TASAF III) awamu ya pili.
Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii wilaya ya Tunduru(Tasaf) Muhidin Shaibu amesema, jumla ya Bilioni 12.4 zimetumika kwa ajili ya malipo kwa walengwa 13,751 wanaonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini katika wilaya ya Tunduru kwa kipindi cha miaka 7 tangu mwaka 2014 hadi kufikia sasa.
Ndg. Muhidin Shaibu alisema,mpango wa kunusuru kaya maskini kwa wilaya ya Tunduru ulianza tangu mwaka 2014 na hadi sasa tayari wameshafanya malipo kwa kipindi cha awamu 32 katika vijiji 88 kati ya 157 vinavyotekeleza mpango huo katika awamu ya kwanza.
Aliendelea kusema shughuli zinazofanywa na walengwa wa kaya maskini ni pamoja na ajira za muda ambapo jumla ya ajira 424 zimeweza kutolewa, ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa vikundi vya wajasiriamali na kazi nyingine za utunzaji wa mazingira, ufugaji wa nyuki, utengenezaji wa mbolea vunde, upandaji wa miti ya matunda, kuchimba visima vya asili na malambo ya kutunza maji, na uchimbaji wa mabwawa ya ufugaji wa samaki.
Alisema kaya 5,111 zimeweza kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa lengo la kujiongezea kipato,kaya 7,670 zimejihusisha na kilimo na ufugaji wa mbuzi,kuku,bata na ng’ombe wakati kaya 5,600 zimefanikiwa kuboresha makazi kwa kujenga nyumba za kisasa.
Hata hivyo mbali na mafanikio hayo baadhi ya walengwa wameweza kuanzisha vikundi 913 vya akiba na mikopo, miradi ya uchimbaji mabwawa ya samaki ambayo imewasaidia kupata ujuzi wa kufuga samaki na kuwa wasambazaji wakubwa wa mbegu za samaki na kitoweo cha samaki ndani na nje ya wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.