Tarehe 22.june 2023 umefanyika mnada wa nne wa ufuta katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru na kufanya jumla ya tani 918 kuingia sokoni kwa mnada huo wa nne .na wanunuzi zaidi ya saba waliomba kununua ufuta huo.
Wanunuzi wanne (04) walifikia lengo la kununua ufuta huo, na kufanya ufuta wote tani 918 kuuzwa katika mnada wa nne kwa bei ya sh 3,497 na kufanya zaidi ya sh. bilioni 3.2 kuingia katika mzunguko wa fedha wilayani Tunduru.
Aidha meneja Masoko TAMCU LTD Ndg Marcelino Mrope amewatangazia wakulima tunu ya mashine za kupulizia kwa bei ya rudhuku ya sh 390,000/=, mashine izo zinapatikana katika chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD).
Mwenyekiti wa TAMCU LTD Ndg. Mussa Manjaule amezidi kuwasihi wakulima kulima mazoa mchanganyiko ili kuweza kujikimu kimaendeleo katika maisha ya kila siku.
Pia kwa upande mwingine afisa ushirika (W) Tunduru Ndg George Bisani amewataka wakulima kuzidi kuongeza nguvu katika kilimo ili kuzidi kufanya maendeleo katika mazingira yetu yao ya kila siku , pia amesisitiza kuzidi kuwepo kwa ushirikiano katika vyama vyao vya msingi ili kujenga ushirika ulio imara.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.