Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametembelea na kukagua ukarabati wa Daraja lililopo Muhuwesi Novemba 12,2023.
Ukarabati huo Mdogo umekuja baada ya daraja hilo kupata hitilafu ya kusogezwa na maji, hali iliyosababisha kutumika kwa upande mmoja wa njia katika daraja hilo,ambapo kwa sasa daraja hilo limesukumwa na kurudi katika hali yake ya hapo awali na kufanya uwezekano wa kutumika kwa njia zote mbili za daraja hilo.
Mkuu wa Mkoa ameipongeza kampuni ya ukandarasi ya Mtivila Traders and Construction ikishirikiana na TANROADS kuweza kukamilisha ukarabati wake na kulirudisha kama awali, ambapo amesema zaidi ya Bilioni 1.5 zimetumika katika ukarabati wa daraja hilo, aidha amewataka wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya Mito ili kulinda miundombinu ya madaraja .
“ Tumekagua na tumejiridhisha daraja limerudi sehemu yake, ni Wajibu wetu kama wananchi ni kutunza miundombinu ya haya madaraja pamoja na barabara zetu”
Mwenyekkiti wa kamati ya siasa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Odo k. Mwisho ameishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za kukarabati daraja hilo, amesema daraja hilo ni kiunganishi muhimu sana baina ya Mkoa wa Ruvuma na mikoa ya jirani ikiwemo Mtwara na lindi, ambapo linawezesha kushirikiana katika biashara baina ya mikoa hiyo.
Akiishukuru serikali ya awamu ya sita Meneja mkuu wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi, Mlima felix Ngaile ameishukuru serikali na kuahidi kuendelea kulinda miundimbinu hiyo kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa ,aidha kwa niaba ya Kampuni ya ukandarasi ya Mtivila Traders and Construction ,Mhandisi Nyoni ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuwaamini wakandarasi wazawa kufanya kazi hiyo , na kuwaomba wakandarasi wazawa kujiamini katika kufanya kazi hizo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.