• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

BIASHARA ya hewa ukaa Mkoani Ruvuma.

Imewekwa : November 8th, 2023

Wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma zimeingia mkataba wa biashara ya hewa ukaa (Carbon) na Kampuni ya Tanzania Carbon(CT Limited) kutoka mkoani Arusha.

Mkataba wa kuanza biashara hiyo umesainiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea chini ya Usimamizi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya CT Limited Marc Backer amelitaja lengo la Kampuni ya Carbon Tanzania kuwa ni kuhakikisha wananchi  wanafaidika kiuchumi na  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupanda miti.

 kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Carbon Limited kutoka mkoani Arusha Marc Backer akizungumza kwenye hafla ya kuweka saini mkataba wa biashara ya hewa ukaa (Carbon) baina ya Kampuni hiyo na wawakilishi kutoka wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma,Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas

Amesema hapa nchini  wananchi wa vijiji nane katika Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameingiza zaidi ya bilioni 2.3 kwa kufanya biashara ya hewa ya ukaa.

“Mradi huu umewanufaisha wananchi wa wilaya za Tanganyika mkoani Katavi na Kiteto mkoani Manyara,hapa Ruvuma mradi wa biashara ya kaboni utakuwa mkubwa sana,tumeshapima tumegundua kuna kaboni nyingi sana’’,alisisitiza Backer.

Backer amesema biashara ya hewa ya ukaa ilianza rasmi mwaka 2018 katika Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi kwa kuendeshwa na  Taasisi ya Carbon Tanzania ambapo mapato ya biashara hiyo yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tunduru Wakili Julius Mtatiro  ameitaja mikataba ya biashara ya kaboni kuwa ina faida kubwa hata kama msitu utatunzwa kwa miaka 60 unaleta faida  kwa wananchi wenye misitu ikiwa ni Pamoja na kuleta mvua nyingi na kwamba wananchi watapata fedha nyingi.

 wakuu wa wilaya za Namtumbo mheshimiwa Ngollo Malenya na Mkuu wa  wialya ya Tunduru mheshimiwa Julius Mtatiro wakiwa na wakurugenzi wa Halmashauri hizo wakiwa kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa biashara ya hewa ukaa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,zoezi hilo lilishuhudiwa na Katibu Tawala wa wa Mkoa wa Ruvuma ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas

Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya amesema biashara ya hewa ukaa ni mradi mpya hapa nchini na kwamba baada ya majaribio katika wilaya ya Tanganyika serikali imeona faida kubwa.

Amesema biashara hiyo inamwezesha mwananchi kupata fedha baada ya kupanda miti ambapo ameitaja wilaya ya Namtumbo kuwa ni wilaya ya kimkakati kwa kuwa asilimia 19 ya maji yanayoingia kwenye mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere Rufiji yanatoka Namtumbo.

Amesisitiza kuwa biashara ya hewa ukaa ni mradi ambao utasaidia kutunza mazingira  na kuhakikisha kuwa uharibifu wa mazingira unakwisha na kwamba mradi utaleta mvua za kutosha na dhana ya Mkoa wa Ruvuma  kuwa ghala la Taifa la chakula itaendelea kuwepo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki  amewaasa wakulima kuhakikisha wananufaika na mradi wa kaboni kwa kuhakikisha wanapanda miti ya kutosha badala ya kuishia kulima mahindi na mazao mengine.

Amewaasa wakulima kupanda miti kwa wingi na kuhifadhi misitu ili kupunguza hewa ya ukaa na kuongeza upatikanaji wa hewa safi lakini pia watakuwa wanafanya biashara ya hewa ya ukaa.

Tanzania imesaini  mikataba ya Kimataifa ambayo inahamasisha biashara ya hewa ya ukaa Duniani ambapo wananchi wanapopanda miti na kuhifadhi misitu inasaidia kufyonza na kupunguza hewa ya ukaa hewani  na kulipwa fedha hivyo kukuza uchumi wao.

Soko la hewa Safi ya Kaboni lililopo ni fursa muhimu kwani Dunia imedhamiria kuboresha Anga kutokana na madhara ya uharibifu wa hewa chafu ya kabon ili kuokoa anga na ongezeko la Joto duniani.

wawakilishi kutoka wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa na Kampuni ya Tanzania Carbon wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini mkataba wa biashara ya hewa ukaa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.