Leo tarehe 10/06/2021 ulifanyika mnada wa 3 wilayani Tunduru. Jumla ya kilo zilizo kuwa zinauzwa leo ni 429,947 na jumla ya kampuni 6 walijitokeza kuomba kununua ufuta wa Tunduru ambao ni
1.RBST international kilo 429,947 kwa kilo 1 Tzs 1800/=
2.MOHAMED enterprise Ltd kilo 200,000 kwa kilo 1 Tzs 2,000/=
3.Lenic kilo 429,947 kwa kilo 1 Tzs 2,070 au Tzs 2,150/=
4.H.S impeksit Tanzania Ltd kilo 200,000 kwa kilo 1 Tzs 2,135/=
5.Yihai Kerry kilo 429,947 kwa kilo 1 Tzs 2,180/=
6.Afrisian Ginning Ltd kilo 429,947 kwa kilo 1 Tzs 2,280/=
Wakulima waliridhia kumuuzia mnunuzi Afrisian Ginning Ltd kilo zote 429,947 kwa bei ya kilo 1 Tzs 2,280/= Sawa na Tzs 980,279,160/=.
Mnada wa leo ulifanyika Kata ya Mchesi, kijiji cha mchesi katika tarafa ya Lukumbule.
Aidha Mnajisi msaidizi wa mkoa wa Ruvuma Bi. BUMI LOGATIANI MASUBA amewataka Wakulima kuongeza bidii ya kulima ufuta na kuacha kutgemea zao moja la korosho tu kama zao la kibiashara hivyo wakulima wa Tunduru waongeze bidii katika kuzalisha zao la ufuta ili likiyumba zao moja la kibiashara wanapata kwenye zao la ufuta.
Pia Wakulima nao wamehaidi kuongeza bidii katika kilimo cha ufuta ili kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Halmashauri kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.