Jumla ya kampuni zilizoshiriki mnada wa leo tarehe 03/06/2021 ni 7 na barua za maombi zilikuwa 7.Aidha jumla ya Tani 251 sawa na kilo 251,000 zimeuzwa kwa mnada wa pili Tunduru, kwa mujibu wa bei ya zilizowekwa sokoni bei ya juu ilikuwa Tzs 2,220/= na bei ya chini ilikuwa Tzs 1,850/=. Baada ya wakulima kuzisikiliza bei zote Wakaamua kuuza kwa kampuni ya RBST COMPANY LTD alieshinda mnada.
Jumla ya kilo 251,000 zimeuzwa kwenye mnada wa leo tarehe 03/06/2021 uliofanyika kata ya Marumba, kijiji cha molandi hivyo jumla ya Thamani ya Tzs 557220000/= ambazo ni fedha zilizoingia kwenye mzunguko wa wananchi na wadau mbalimbali wa zao la ufuta Tunduru.
Aidha tozo ya usafiri itategemea na umbali kutoka alipo mkulima wa ufuta wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Pia mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Tamcul Ndg Mussa Athumani Manjaule amewataka wakulima hao wa ufuta waongeze bidii katika kulima zao hilo la ufuta maana litakuwa mkombozi katika maisha yao ya kila siku uku vipato vyao kiuchumi vitapanda aidha mwenyekiti aliwataka wakulima wajitaidi kushirikiana vizuri na wadau wa bank mbalimbali zinazo patikana katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa sababu wadau hao wa Bank ni wadau muhimu sana kwa wakulima.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.