Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru wamefanya baraza la robo ya nne kwa mwaka wa fedha ulioishia juni 2023 tarehe 27/08/2023 katika ukumbi wa mikutano claster uliopo Tunduru.
Mkutano huo wa baraza ulihudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani , Mkuu wa wilaya ya Tunduru ,Mkurugenzi mtendaji, Ofisi ya RAS ,Wakuu wa idara na vitengo na Maafisa tarafa.
Akizungumza, Mwenyekiti wa mkutano Mheshimiwa Hairu Mussa ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru , ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa ,Dkt. Samia suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa ya kuendelea kuinua maendeleo katika wilaya ya Tunduru.
"Tunaishukuru serikali kwa kutuletea miradi mingi ambayo haijawahi tokea kwa kipindi cha nyuma". Alisema.
Aidha Mheshimiwa Hairu amewasisitiza wataalamu ,kuzidi kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato kwa ukaribu ili kuongeza mapato, ambayo yanakwenda kukamilisha miradi yetu ya maendeleo iliyopo katika kata na vijiji.
Vile vile amesisitiza idara ya kilimo maafisa ugani kuwa na karibu na wakulima ,ili kuweza kuwasaidia mbinu bora za kuweza kuongeza uzalishaji, hasa katika mazao haya ya biashara katika wilaya yetu ya Tunduru.
Aidha, Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro, amesisitiza katika kuongeza vyanzo vya mapato katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru , na kuangalia fursa mpya zitakazoweza kuongeza ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Vile vile Mhe. Mtatiro amewataka madiwani kusimamia kwa ukaribu suala la ufugaji holela wakishirikiana na watendaji wao wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wananchi kutouza maeneo yao yanayosababisha kukaribisha ufugaji holela katika wilaya yetu.
"Ninyi ni wawakilishi wa wananchi katika maeneo yenu,tukaongeze nguvu ya mikutano na watendaji wetu, tusaidiane kusimamia ili kuondoa ufugaji holela " alisisitiza Mhe. Julius Mtatiro.
Baraza la madiwani liliambatana na uchaguzi wa viongozi ngazi kuu tatu,kamati ya maadili ambayo itaongozwa na Mh. Hamisi Kaesa Diwani wa kata ya Matemanga, kamati ya Uchumi itaongozwa na Mh. Ado Saidi Tima Diwani kata ya Mchesi, na kamati ya huduma za jamii itaongozwa na Mh. Stawa Timamu Diwani viti maalumu kata ya Matemanga.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.