Halmashauri yakabidhiwa kompyuta kwa ajili ya kurahisisha kukusanya na kuripoti taarifa za watoto,
akizungumza wakati wa makabidhiano meneja wa mradi wa PACT kanda ya kusini bi Mary Marandu alisema kuwa asasi yao imefanikiwa kutoa kompyuta 17 katika halmashauri 17 zilizopo chini ya mradi wa kizazi kipya kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa data za watoto wenye matatizo mbalimbali kama shinikizo la damu (hypertension), na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri (W) Ndg Abdallah H Mussa amewashukuru kwa uwezeshaji huo na kuitaka Idara ya Afya kupitia kitengo cha ustawi wa jamii kutumia vifaa hivyo kwa kazi husika na kuhakikisha kuwa taarifa zote zinazohusiana na watoto zinakusanywa kwa usahihi na wakati ili kufikia lengo la kupata kanzi data ya watoto wenye mahitaji muhimu katika jamii na kurahisha upatikanaji wa huduma.
Meneja wa mradi wa PACT kanda ya kusini Bi Mary Marandu akitoa maelezo ya taasisi yao kwa Mkuregenzi Mtendaji (W) Ndg Abdallah H Mussa wakati walipofika katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kukabidhi kompyuta kwa ajili ya ukusanyaji wa data za watoto katika mradi wa kizazi hai mapema wiki hii
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.