• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

AFISA MAZINGIRA AKERWA NA TABIA ZA UCHOMAJI MOTO

Imewekwa : August 24th, 2017

Aliyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa maeneo yaliathiriwa na wafugaji wenye makundi makubwa ya mifugo waliopo katika maeneo tofauti ya wilaya ya Tunduru.

Mkuu wa Idara ya Mazingira na Uthibiti wa Taka Ngumu wilaya ndg Jonathan Albano Haule alisema kuwa imekuwa kawaida ya wananchi kusafisha mashamba kwa kuchoma moto hali inayohatarisha uharibifu wa misitu ya asili na kuharibu mazingira kwani unapochoma moto katika mazingira unaua mimea yote.

Aliendelea kusema kuwa sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 inasema Mtu yeyote anayeishi Tanzania atakuwa mdau na atawajibika kutunza nakuendeleza mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu shughuli au jambo lolote ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kuathiri mazingira.

uthibiti wa mazingira ni wajibu wa kila mtu ili kuhakikisha kwamba nchi inapambana na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanaathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji kushuka kutokana na kukosekana kwa mvua na ongezeko kubwa la hali joto.hivyo basi ni wajibu kwa kila kiongozi katika ngazi ya kata, kijiji hadi wilaya kuhakikisha kuwa mazingira yanalindwa na kupiga vita uchomaji wa nyasi wakati wa maandalizi ya mashamba ili kuepuka athari zinazosababishwa na moto.

Akiwa katika tarafa ya Nakapanya, kata za Mindu, Tinginya na Ngapa aliwaagiza viongozi wa sehemu hizo kufuatilia na kuwachukulia hatua wananchi wanaochoma moto katika mashamba kwani wanasababisha madhara mengi sana katika mazingira.

Aliendelea kusema kuwa kutokana na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji  kama kilimo, kulisha mifigo na zimepelekea ongozeko kubwa na kukauka kwa vyanzo vya maji na uharibifu wa uoto wa asili katika mito mingi hivyop kupelekea  kukauka na inakuwa na maji kwa msimu tu wa mvua hali inayoatarisha maisha ya wananchi hasa upatikanaji wa maji safi na salama.

Vile vile kumekuwa na ongezeko kubwa la kundi kubwa la mifugo katika wilaya ya Tunduru, mifugo hii inaathiri kwa kiasi kikubwa mapori ya asili katika vijiji na mapori tengevu ya hifadhi za taifa kwani wafugaji hawa wanavamia katika misiti na kukata miti kwa wingi ili kuruhusu nyasi ziote kwa ajili ya malisho.

Afisa Mazingira na Mthibiti wa Taka Ngumu W ndg Jonathan Haule akitoa elimu ya umuhimu wa kutunza mazingira na ufugaji endelevu, faida zitokanazo na ufugaji katika kata ya Ngapa wakati wa ziara ya kuzungumza na wananchi juu ya athari zinazosababishwa na wafugaji wenye makundi makubwa ya ng'ombe wliovamia katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru.



Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.