Afisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Tunduru,Ndg, Morton Msowoya amehamasisha wakulima wa wilaya hiyo kujiandikisha kwaajili ya kupata pembejeo za kilimo katika kuajiandaa na kilimo katika msimu huu.
Akizungumza na wakulima katika kijiji cha Ligunga,wakati wa mnada wa nane wa Korosho, ndg Msowoya alisema kuwa serikali inaendelea kutoa pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa ajili ya kuwawezesha kuzalisha mazao kwa wingi na kupata mavuno bora.
"Ninawasihi wakulima wote kujitokeza Kwa wingi kujiandikisha na kuhuisha taaarifa zenu kwaajili ya kupata pembejeo za kilimo," alisema Msowoya. "Pembejeo hizi Ni muhimu Kwa ajili ya kilimo chenye tija."
Kwa upande wake, Afisa Ushirika Wilaya ya Tunduru, Ndugu George Bisani, amesisitiza vyama vya ushirika vya msingi kulipa wakulima Kwa haraka ili hizi fedha ziweze kubadili maisha yao na kuyaendesha Kwa usahihi.
Ndg.Bisani Bisani, alisema kuwa zaidi ya bilioni 45 ziliingia kwenye mzunguko kupitia zao la korosho katika mikoa mitatu ambayo chama kikuu cha ushirika Tunduru TAMCU LTD kinahudumia.
"Ni muhimu kwa vyama vya ushirika vya msingi kulipa wakulima kwa haraka ili fedha hizi ziweze kusaidia wakulima katika shughuli zao za maendeleo," alisema ndg.Bisani.
pichani: Afisa Ushirika Wilaya ya Tunduru, Ndugu George Bisani
Aidha Afisa Ushirika Wilaya ya Tunduru amevipongeza vyama vya Msingi vya Ushirika Kwa utendaji kazi wa ukusanyaji wa mazao hasa katika msimu huu wa zao la korosho.
Katika msimu huu wa zao la korosho, jumla ya minada nane imefanyika, ambapo zaidi ya tani 26,000 zilikusanywa na kufanya zaidi ya Bilioni 45 kuingia katika mzunguko katika mauzo ya zao hilo la korosho.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.