MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA BAJETI YA MWAKA 2022/23
1 SEKTA YA ELIMU MSINGI
Elimu Msingi bila malipo inaendelea kutolewa kwa wanafunzi, Walimu na Walimu Wakuu wamelipwa stahiki zao. Mpango wa Boost umeendelea kutekelezwa baada ya wataalam kupata mafunzo ya namna ya kusimamia mradi huu. Mradi unatekelezwa kwenye shule Saba (7) badala ya 26 zilizopitishwa kwenye Bajeti kutokana na hitaji la serikali la kuhakikisha changamoto za miundombinu ya elimu zinamalizwa kwenye shule zote kwa awamu. Shilingi 1,224,600,000.00 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kawaida 38, madarasa ya awali ya mfano 6 na vyoo matundu 61.ujenzi wake umefikia hatua ya umaliziaji. Halmashauri imesimamia ujenzi wa madarasa 2 S/M Nandembo pamoja na ya ujenzi ya darasa moja klasta ya Nampungu. Aidha fedha za kukamilisha maboma zimepokelewa shilingi 599,250,000.00 mwishoni mwa mwezi sita na zipo mashuleni kwenye miradi na zitatekeleza miradi kuanzia Julai 2023
2 SEKTA YA ELIMU SEKONDARI
Elimu Msingi bila malipo inaendelea kutolewa kwa wanafunzi, Walimu na wakuu wa Shule
Utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa hostel 2, madarasa 14, Mabweni 7 unaendelea kwenye hatua za kuezeka kwenye sekondari za Masonya na Tunduru kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu 2023, ifikspo tarehe 10/08/2023. Aidha, Ujenzi wa shule mbili mpya za Tinginya na Tuwemacho maandalizi yanaendelea.
3 SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII
Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF unaendelea kufanyika ambapo malipo ya ruzuku na kazi yametolewa ambapo jumla ya shilingi 3,517,510,899.00 zilipokelewa na kutumika na ruzuku wa wanufaika, ununuzi wa vifaa vya kazi. Aidha, utekelezaji wa miradi ya PWP upo kwenye hatua ya kuibua miradi mipya na kukamilisha miradi ya mwaka 2022/23 ambapo wanufaika wanashiriki kazi mbalimbali zikiwemo ujenzi wa barabara, kazi za kilimo cha mashamba zinafanyika na wanalipwa kwa siku walizofanya kazi.
Mikopo laini kwa vikundi yamefanyika kwa vikundi ambapo shilingi 281,168,181.75 zimekopeshwa kwa vikundi viiwemo vya walemavu 7 vilivyokopeshwa shilingi 57,233,636.35, wanawake 15 vilivyokopeshwa shilingi 112,467,272.70 na vijana vikundi 13 vilivyokopeshwa shilingi 114,467,272.70 kufikia Juni 2023. Mikakati ya kukusanya madeni inaetekelezwa kwa kuvifuatilia vikundi vyote vilivyokopa kwa ushirikiano na Polisi kwa vikundi vnavyoonyesha kutoshirikiana
Idara hii inaendelea kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kuhamasisha shughuli za maendeleo kwenye vijiji mbalimbali vya Tunduru
4 SEKTA YA UTAWALA
Mafunzo ya Waheshimiwa Madiwani 54 wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wameshiriki mafunzo kwa vitendo katika ziara ya mafunzo iliyofanyika Agosti 2022 huko Mbeya kwa kujifunza ukusanyaji wa mapato ya ndani katika H/W ya Mbalali, Njombe pamoja na kujifunza kwa kukagua mabanda ya maonyesho kweye Maonyesho ya nanenane.
Ukarabati wa jengo la Halmashauri umefanyika kwa kupaka rangi nje ya jengo pamoja na kurekebisha mfumo wa Vyoo wa Jengo hili.
5 SEKTA YA AFYA
Ujenzi wa jengo la Hospitali ya wilaya unaendelea kwa kukarabati jengo la upasuaji na kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na maabara. Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nakayaya, Masonya, Mchesi, Nalasi na Nampungu umeendelea kutekelezwa katika hatua tofauti za ujenzi na ukamilishaji. Aidha, Zahanati za Mwongozo, Angalia, Namasalau, Likweso, Malombe, Naluwale, Darajambili na Chiungo umeendelea katika hatua za umaliziaji. Kituo cha Afya cha Nalasi na Masonya vimepelekwa vifaa vya awali ili vianze kutoa huduma baada ya kuingiza umeme kutokana na hitaji kubwa la kufunguliwa vituo hivi.
Utekelezaji wa shughuli za Lishe Wilayani umefanyika kwa kuendesha vikao vya Kamati ya Lishe katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.