kibali cha Ujenzi .
Ili kupata kibali cha ujenzi katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru mwananchi unatakiwa kuwa na vitu/ nyaraka zifuatazo;-
1.Hakikisha kuwa una kiwanja kilichopimwa
2. Andaa michoro ya ujenzi kwa kuwatumia wataalam wanaokubalika kisheria ambao ni wasanifu majenzi, wahandisi au wakadiriaji majenzi.
3.Hakikisha michoro ya ujenzi imehakiiwa na wataalamu (Halmashauri husika)
katika halmashauri ya Tunduru kuna wataalamu mbalimbali wanaohakiki na kuhakikisha unapata kibali cha ujenzi kama ifuatavyo;-
a. Afisa Ardhi kuhakiki mmiliki halali wa kiwanja na kama kiwanja kinachoombewa kibali kipo.
b.Afisa mipango Miji ambaye atahakikisha kuwa matumizi bora ya ardhi yanafuatwa, mfano kama kiwanja ni cha makazi pekee, makazi na biashara, viwanda, eneo la wazi, huduma za jamii.
c Afisa Mazingira kuhakikisha kuwa mchoro unazingatia athari za kimazingira.
d.Afisa Afya- kuhakikisha kuwa michoro imezingatia afya za watumiaji.
e. Mhandisi ujenzi (Strucutre Engneer) -kuhakikisha kuwa mchoro umezingatia uimara wa majengo/ jengo, kufanya uhakiki zaidi kwenye michoro ya kihandisi (structuredrawings). mfano ukubwa na aina za nondo, kina cha msingi kulingana na eneo husika. -changamoto kubwa ambazo zinaweza kutoka kwenye majengo marefu (maghorofa).
f. Msanifu majengo (Archtecture) - kuhakikisha kuwa michoro inayokusudiwa kujengwa imekidhi viwango vya kitaalam (specifications). mfano kuhakikisha kuwa michoro inayowasilishwa imekamilika na kukidhi viwango.
g. Mkadiriaji majenzi (quantity surveyor) -kutoa ushauri kuhusiana na gharama ya jengo linalokusudiwa kujengwa.
Baada ya michoro hiyo kuhakikiwa na wataalam wa mamlaka ya halmashauri ya Tunduru kama walivyooredheshwa hapo juu mhandisi ujenzi hutoa kibali cha ujenzi baada ya kuhakikisha kuwa wataalam wamehakiki na yeye mwenyewe kujiridhisha.
Kama kuna eneo ambalo michoro haijakidhi vigezo kwa mujibu wa wataalam, marekebisho lazima yafanyike ndipo kibali cha ujenzi kitolewe.
NB. Taratibu za utoaji wa vibali vya ujenzi unaweza kutofautiana kidogo kati ya mamlaka moja na nyingine kutokana na taratibu mamlaka hiyo na watumishi waliopo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.