Wilaya ya Tunduru ina vivutio vingi vya utalii na malikale, Misitu ya Asili,Hifadhi ya Taifa ya Selous,Utamaduni na Hifadhi mbalimbali za malikale zinazopatikana katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Tunduru
vivutio hivi vinaweza kuiingizia Wilaya ya Mapato na kuongeza pato la taifa, ndani ya Halmasahuri ya wilaya ya Tunduru kuna malikale ambazo ni kielelezo cha utamaduni wa wakazi wa Tunduru, kama vile malikale ya hifadhi ya Masonya ambayo ni kambi iliyotumiwa na wanaharakati wa Msumbji wakati wa ukombozi kutoka katika utawala wa Ukoloni wa Mreno,