Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeanzisha shamba darasa la ufuta lenye ukubwa wa ekari mia moja kwa lengo la kuongeza kipato cha Halmashauri pia ni shamba darasa kwa wakulima wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Aidha shamba hilo la ufuta lililopo katika tarafa ya lukumbule kata ya lukumbule kijiji cha lukumbule ambalo kwa sasa ufuta umefikia hatua zuri ya kuchanua uku maafisa kilimo ngazi ya kata wakitakiwa kwenda site kuwafundisha wakulima mbinu bora ya kilimo cha kisasa katika zao la ufuta ili kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja, Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Aidha malengo ya Halmashauri ni kuhakikisha zao la ufuta nililimwe kwa wingi katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru zao la ufuta litasaidia sana kunyanyua uchumi wa Wakulima wa Halmashauri wa wilaya ya Tunduru uku zao la kwanza la biashara la wakulima wa Tunduru ikiwa ni zao la korosho.
Pia kutokana na Wanyama pori Waharibifu aina ya Tembo Wakulima wa Tunduru wameshauriwa na wataalamu wa kilimo kuwa waelekeze nguvu zao kulima zao la ufuta maana Tembo hawezi kula ufuta pia baada ya mkulima kuvuna ufuta na kupeleka kuuza stakabadhi gharani na kupata pesa ambazo zitawasaidia kununua mahindi na mazao mengine ya chakula.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.