Waziri Mkuu Atoa Katazo la Wananchi Kuacha Tabia Ya Kukata Miti -Kalulu
Akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha mbungulaji kilichopo kata ya Kalulu wilayani Tunduru, unaotekelezwa kwa mchango wa Halmashauri katika miradi ya maendeleo,wananchi pamoja na serikali kuu.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rahaleo baada ya kupokea taarifa ya utekelezajiwa mradi wa uchimbaji wa visima viwili virefu katika kijiji cha Mbungulaji na Rahaleo waziri mkuu alisema serikali inatekeleza kwa vitendo sera ya ilani ya chama cha mapinduzi na imeanza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha kuwa kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama.
Na ili serikali iweze kufikia malengo hayo na kutunza vyanzo maji ni lazima wananchi kutunza mazingira na kuacha tabia ya kukata misitu ovyo kwani hali ukame maeneo mengi yanachangiwa na uharibifu wa uoto wa asili.
Waziri Mkuu akitoa maekelezo kwa wananchi na watumishi wa serikali wakati akiwa katika ziara mkoani Ruvuma, hapa ni katika kijiji cha Mbungulaji kata ya kalulu wilayani Tunduru.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliwataka wananachi kutunza mazingira na kucha tabia ya kufanya kilimo katika vyanzo vya maji na katika mabonde ambayo ni hifadhi ya maji
Vilele vile Mh. Majaliwa alisema serikali imeweka fedha nyingi sana katika miradi ya maji katika kijiji cha mbungulaji na Rahaleo hivyo ni jukumu la wananchi kusimamia miundombinu hiyo ya maji na kuhakikisha kuwa baada ya mradi kukamilika unakuwa endelevu kwa kutunza mazingira yanayozunguka visima vya maji.
Alisema waziri mkuu “jumla ya milioni 112 laki 226 mia 290 zimtengwa na serikali ya halmashauri kugharimia mradi huu hivyo ambapo katika kijiji cha mbungulaji shilingi milioni 28 laki 217 mia 660 zitatumika na katika kijiji cha rahaleo milioni 84 na elfu 9 mia 260 zitatumika”
Nimeelezwa kuwa mradi huu utawafikiwa wakazi wapatao 4,879 ambapo kati ya hao Mbungulaji wakazi 1,799 na Rahaleo wakazi 3,080, na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika vijiji hivi kwani wananchi wanategemea visima vitatu tuu vinavyofanya kazi kwa sasa huku visima 15 miundombinu yake ikiwa imechakaa na visima vingine kukosa maji kutokana na kina cha maji kupungua, hali inayochangiwa na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili
kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya Tunduru Ndg Chiza C Marando akisoma taarifa ya utekelezaji uchimbaji wa visima virefu vya maji katika kijiji cha Mbungulaji kwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa wakati akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kukagua ukamilifu wa barabara ya Lami inayoungana wilaya za Tunduru-Mangaka na Tunduru Namtumbo iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika kwa asilimia 100.
Viongozi wa vijiji vyote hakikisheni kuwa katika maeneo ya kuzunguka kisima miti ya kuhifadhi maji inapandwa mita 100 kuzunguka eneo hilo kila upande ili kulinda visima hivi visikauke na kukosa huduma ya maji alisema waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mhe.Kassimu Maliwa.
Aliendelea kusema kuwa serikali inatakeleza miradi mikubwa ya maji vijiji inayoendeshwa na serikali kwa ufadhili wa benki ya dunia na Tunduru miradi hii inatekelezwa katika vijiji kumi, kuna mradi wa maji Lukumbule, Mtina,Matemanga, Mbesa, Amani ambayo ipo katika utekelezaji.
Waziri Mkuu wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. kassimu Majaliwa akisamia wananchi alipowasili katika kijiji cha Mbungulaji kata ya Kalulu wilayani Tunduru akitokea wilaya ya Namtumbo, kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera na Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme.
Waziri mkuu alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua wakandarasi ambao wanafanya miradi kwa kususua ikiwa ni pamoja na kuvunja mikata yao mara moja, hata hivyo alitoa muda wa wiki mbili kwa kampuni za wakandarasi wa maji katika mradi wa mtina na matemanga kukamilsha kazi ya ujenzi wa miradi hiyo kabla ya serikali kuwachukulia hatua.
Waziri mkuu Kassimu Majaliwa aliwaagiza viongozi wa wilaya kuwapa hao wakandarasi wiki mbili tu kama watakuwa hawajamaliza kazi kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kusitisha mikata yao mara moja.
Waziri Mkuu Mh.Majaliwa Kassimu Majaliwa akitoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya juu ya utunzaji wa mazingira kuzunguka vyanzo vya maji kwa kupanda miti mita mia kila upande kuzuia kukauka kwa vyanzo hivyo kutoka na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.