Tusesco ni Umoja wa Waitimu katika Shule ya Sekondari Tunduru ambao waliitimu miaka ya 1985 adi 1990 ambapo Mwenyekiti wa Tusesko Bw.John Maongezi amesema “Jumuiya ya Tusesko tangu ianzishwe kupitia Wanachama wake inachangishana fedha kwa lengo la kutatua matatizo mbalimabali yanayo ikabili shule hiyo ya Tunduru sekondari ambapo kabla ya kuandaa meza na seti za viti walichukua mawazo ya Walimu ili kuangalia kipi ni kipao mbele cha shule kwa sasa ndipo jibu likapatikana kuwa kuna upungufu wa seti za Meza na viti kwaiyo jumuiya ikaona ni vizuri kuchonga seti za Meza na viti 45”.
Aidha Tusesco kupitia Mwenyekiti wake imesema nia ya kuendelea kuichangia Tunduru sekondari bado wanayo na malengo ya kuhakikisha shule yao ya Tunduru sekondari inaendelea kuwa na miundombinu na Taaluma bora bado wanayo sababu vipaumbele bado wanavyo pia kutoa hamasa kwa wanafunzi ambao wanaoendelea kusoma na waliomaliza katika shule hiyo wawe na moyo wa Uzalendo wa kuipenda shule yao.
Kwa Upande wake Mkuu wa Shule Tunduru Sekondari Bw.Namlya Ismaili amesema “Nawashukuru sana Waitimu waliomaliza tangu shule inaanzishwa adi miaka ya 1990 kwa wao kujitoa kwa Uzalendo wao wakuonyesha nia ya kuiunga mkono serikali kwa kuipatia Tunduru Sekondari seti za meza na viti 45 vyenye gharama ya Shilingi Milioni tatu laki sita na ishirini elf ( Tzs.3,620,000/=) uku akihaidi kuwa watatunza Vitu vyote vya shule ikiwemo na misaada mbalimbali wanayo patiwa na wadau wa maendeleo kama hao Waitimu wa zamani katika Shule hiyo”.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Julius Mtatiro kwa upande wake baada ya kupokea msaada huo wa seti za meza na viti kutoka kwa Waitimu hao wa zamani katika Shule ya Sekondari Tunduru amesema “Walichokifanya Tusesco ni kuunga mkono jitiada zinazofanywa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuhakikisha kuwa miundombinu ya kusomea Wanafunzi wetu inakuwa bora ikiwemo kupata hizo seti 45 za meza na viti ambazo Tusesko wametoa katika shule yao pendwa waliosoma tangu inaanzishwa adi miaka ya 1990” pia Mkuu wa wilaya ya Tunduru amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw.Sostenes Bwilo kuwa iandaliwe Cheti maalum ambayo itakuwa na majina ya Watu wote wa TUSESCO ambao ni Wanafunzi wa zamani wa Tunduru sekondari kwa Uzalendo wao wamejitolea seti 45 ya meza na viti kwahiyo cheti hicho kitasainiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Pia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bw. Sostenes Bwilo wakati akimkabidhi Mkuu wa shule ya Sekondari Tunduru Bw.Namlya Ismaili seti 45 ya meza na viti amemtaka kutunza vizuri mali hizo za shule ili ata kipindi kijacho walioisaidia shule hiyo watakapo fika tena wazikute mali za shule zipo salama lengo waendelee kuwa na moyo wakuisaidia zaidi shule hiyo ya Tunduru Sekondari.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.