TASAF YATOA MALIPO AWAMU YA 20
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inaendelea na zoezi la kugawa ruzuku kwa walengwa wa Tasaf iii wapatao 14,516.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji kaimu mratibu wa Tasaf wilaya ndg Muhidin Shaibu alisema kuwa watafanya malipo ya jumla ya shilingi milioni 402,344,000 katika awamu ya 20 ya malipo.
Kaimu mratibu Tasaf wilaya aliendelea kusema kuwa ruzuku hiyo inalenga katika Elimu, Afya na Kujikwamua kiuchumi kwa walengwa ili kuachana na umaskini.
Aidha alisema kuwa malipo yatafanyika kwa muda wa siku NNE kuanzia tarehe 30/mei hadi tarehe 02/June 2017 katika vijiji 88 vilivyopo katika mpango.
Muhidin Shaibu aliendelea kusema kuwa wanufaika watapewa mafunzo ya namna ya kutumia ruzuku kwa manufaa ya kujikomboa na umaskini,pamoja na kusikiliza changamoto zinawakabili wanufaika wa Tasaf.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.