Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,
ametoa maagizo kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi ambaye
pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, kuhakikisha ndani ya siku tano soko la
Kata ya Nakapanya wilaya ya Tunduru mkoani humo linafungliwa na kuanza
kutoa huduma kwa wananchi.
Maagizo hayo aliyatoa jana wakati akizungumza na wakazi wa kata hiyo
muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku
tano akitokea mkoa wa Mtwara.
Rais Magufuli alifikia maamuzi hayo baada ya wananchi kutoa kilio chao
cha muda mrefu cha kukosa sehemu ya kufanyia biashara huku wakiwa na
jengo ambalo lilishajengwa kwa kipindi cha miaka saba iliyopita,kwa
madai kuwa jengo hilo lipo karibu na kituo cha Mahakama ya mwanzo.
“Mkuu wa mkoa nataka ndani ya siku tano jengo hili liwe limefanyiwa
uboreshwaji na lianze kutumika ili kuwaondolea adha wananchi waliokuwa
wakiipata kwa muda mrefu sasa”alisema Rais Dkt.John Magufuli.
Aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli aliutaka uongozi wa Mahakama
Wilaya ya Tunduru kutafuta eneo lingine la kujenga kituo cha Mahakama
ili kuacha huru eneo hilo kwa shughuli za biashara.
Magufuli ambaye alilazimika kutembelea eneo hilo la soko pamoja na
jengo la kituo cha Mahakama ya mwanzo Nakapanya,ambapo alisema kuna
kila sababu ya kujenga kituo kipya cha Mahakama kutokana na jengo la
awali kuwa na uchakavu.
Hata hivyo akiwa kwenye majengo hayo alitoa shilingi milioni kumi huku
viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge walichangia milioni 12 na kufanya
jumla ya shilingi milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha
Mahakama.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.