Muungano wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (CWMAC) ikishirikiana na shirika la Honeyguide wameeendesha mafunzo ya usimamizi endelevu wa Maliasili ya jamii kwa viongozi wa Jumuiya za Hifadhi kupitia mradi wa Kujenga Usimamizi wa Asili (KUWA) katika Wilaya ya Tunduru.
Lengo la mafunzo haya ni kujenga uelewa wa viongozi wa jamii kuhusu masuala yanayoweza kuathiri uendelevu wa jumuiya zao katika Uchumi, Jamii, na Mazingira, hayo yamesemwa na Afisa mjenga uwezo wa Muungano wa Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori Tanzania Ndg. Prosper Munisi
Mafunzo hayo yameendeshwa kwa siku zisizopungua nne , kwa Jumuiya mbili za hifadhi ambazo ni Jumuiya ya Chingoli na Kisungule ,mafunzo haya yalihudhuriwa na makundi mbalimbali Wanawake,Wanaume, Vijana na Wazee.
“Wananchi wamepewa dhamana kubwa sana na Mkurugenzi wa Wanyamapori Tanzania ,ili waweze kufanya uhifadhi wa Wanyamapori na kufadika na rasilimali walizonazo kwa kizazi cha sasa na baadae”.Alisema.
Aidha Afisa Wanyamapori (W) Tunduru Ndg. Dunia Almasi amesema mafunzo haya ni muhimu sana kwani yanakwenda kuwaimariasha viongozi katika usimamizi wa rasilimali za jamii , pia mafunzo hayo wakayafikishe kwa jamii kwani ni jukumu lao la kwanza kama viongozi.
Wilaya ya Tunduru ina jumla ya jumuiya mbili za Hifadhi Wanyamapori ambazo zimekwishapata mafunzo hayo ambazo ni Jumuiya ya Narika na Chingoli pia kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma jumla ya jumuiya tano zimekwishapata mafunzo hayo.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano serikalini Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.