Maafisa kutoka Kitengo cha Ustawi wa Jamii,Idara ya Maendeleo ya Jamii na Dawati la Jinsia na watoto watoa elimu ya Jinsia, Haki za Mtoto pamoja na Makatazo ya kisheria kwa watoto. Wanafunzi kutoka Shule tatu za Sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru walipokea Elimu hiyo, shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Matemanga, Shule ya Sekondari Kiuma, Shule ya Sekondari Namwinyu. Juhudi hizi kubwa zinalenga kuwalinda na kuwaelimisha wanafunzi kuhusu masuala muhimu ya jinsia na haki zao.
Mtaalamu kutoka Jeshi la Polisi, Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto, Koplo Humphrey, alitoa elimu kuhusu jinsia na makatazo ya kisheria kwa wanafunzi. Elimu hii ililenga kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu masuala ya kijinsia na kuwafanya waweze kutambua na kuzuia aina zote za ukatili na unyanyasaji.
Baada ya elimu hiyo, wanafunzi wa kike walipokea Sodo/Pedi kutoka kwa wadau wa maendeleo, taasisi ya PARMS FOUNDATION/NALIKA. Watoto wa kike walipewa elimu kuhusu Hedhi Salama na namna bora ya kutumia Sodo/Pedi wakati wa hedhi, ili kuhakikisha kuwa wanakuwa salama na wanahudhuria shule bila vikwazo.
Elimu hii iliyotolewa itasaidia kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu masuala ya jinsia na haki za mtoto. Wataweza kutambua haki zao, kujilinda dhidi ya ukatili na unyanyasaji na kuwa na maisha bora.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.