Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Julius Mtatiro amefungua Mafunzo ya Waheshimiwa Madiwani ambapo Mafunzo hayo ya siku mbili Waheshimiwa Madiwani Watajifunza Mada mbalimbali ambazo zinausiana na maswala mbalimbali ya kiuongozi.
Dc Mtatiro amewataka Waheshimiwa Madiwani kuwa Wasikivu kwa kile watakacho fundishwa na Wakufunzi kwani kile kitakacho fundishwa ni muhimu sana kwao kwa sababu itawasaidia kufanya kazi zao za uongozi kwa weledi na kuwashirikisha Wataalam na Wananchi kwa ujumla.
Aidha Mkuu wa Wilaya aliwataka Waheshimiwa Madiwani katika maeneo yao ya Kiutawala wakajitaidi kuwasimamia Watendaji wa Vijiji na Kata kuhakikisha wanakusanya Mapatao ambapo Mkuu wa wilaya alisema Zao la Mpunga ndio zao linalo fuata kwa uzalishaji ukiondoa Korosho Wilaya ya Tunduru kwahiyo jukumu la kusimamia mapato sio la Dc au Mkurugenzi peke yake.
Pia Mkuu wa Wilaya aliwaeleza Waheshimiwa Madiwani na Wageni waalikwa kuwa kamati ya ulinzi na Usalama inasubiria mitihani ya kidato cha nne imalizike ndipo opresheni ya kuondoa mifugo iliyo ingia wilaya ya Tunduru bila kibali itaendelea hivyo amewataka Waheshimiwa Madiwani kwa kushirikiana na Wananchi watoe taarifa mapema pale wanapo iona mifugo mingi kwenye eneo ambalo halina kitalu kwajili ya Wafugaji.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.