WAKULIMA wa Mbaazi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wameingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.69 baada ya kuuza Kilo 839,940 za mbaazi katika Mnada wa kwanza Msimu wa mwaka 2022/2023.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Oparesheni wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) Bw. Marcelino Mrope wakati akizungumza na Wanahabari ofisini kwake Mjini Tunduru.Bw, Mrope amesema TAMCU katika msimu wa Mwaka 2023/2024 imejiwekea malengo ya kukusanya Mbaazi Kilo 5,350,788 na kwamba katika msimu huu Chama kimeagiza viroba 130,000 kwa ajili ya kuhifadhia Mbaazi.
Hata hivyo, amesema kuwa ukusanyaji wa Mbaazi katika msimu wa 2022/2023 uliendelea kuuzwa kwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani, ambapo jumla ya Minada sita ilifanyika na Kilo 3, 035,692 ziliuzwa na kuwaingizia Wakulima zaidi shilingi bilioni 2.6.
“ukusanyaji wa zao la Mbaazi umepungua kidogo kutoka kilo 4,111,845 msimu wa mwaka 2021/2022 hadi kilo 3,035,692 msimu wa mwaka 2022/2023 ambapo ni sawa na anguko la asilimia 26.17 la ukusanyaji katika mauzo”, alisema.
Mnada wa pili wa zao la Mbaazi Wilayani Tunduru unatarajia kufanyika katika kijiji cha Msinji Agosti 24, 20
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
BILIONI 1.2 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA AFYA TUNDURU
Serikali ya awamu ya sita imetoa bilioni 1.2 kuboresha miundombinu ya hospitali kongwe iliyoanzishwa mwaka 1930 wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.
Mganga mfawidhi wa hospital ya wilaya ya Tunduru, Daktari Athumani Mkonoumo amesema wamepokea shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya hospitali hiyo ambayo inajenga maabara mpya, Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na chumba cha upasuaji.
Amesema Serikali pia imetoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo ya wagonjwa wa Dharura (EMD), na kwamba limekamilika na kuanza kutoa huduma za dharura tangu Juni mwaka huu.
Vilevile, hospitali imepokea vifaa vya matibabu katika jengo hilo la dharura (EMD), vifaa hivi ni pamoja na Mashine ya X-Ray, Utrasound na mashine za kusaidia kupumua pamoja mitungi ya gesi ambapo hadi sasa wagonjwa zaidi ya 86 wamefanikiwa kupatiwa huduma zinazotolewa na EMD.
“Itatusaidia sana kutoa huduma bora na stahiki kwa sababu hatutokua na changamoto kubwa ya vifaa na miundombinu sahihi ya kutoa hizo huduma”. Alisema.
Ukarabati huu mkubwa wa hospitali utapunguza idadi kubwa ya wagonjwa kupewa rufaa ya kwenda kupata huduma nje ya wilaya.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
22/08/2023.
Kaimu Afisa Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Dastan Chiyombo amesema Serikali imetoa Zaidi ya Shilingi billion 1.2 kutekeleza miundombinu 83 katika Shule za msingi.
Chiyombo amesema hayo mjini Tunduru katika mahojiano maalumu ambapo amesema fedha hizo zimetolewa kupitia programu ya BOOST na kwamba utekelezaji wa miradi hiyo ipo katika hatua za umaliziaji.
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.