TAARIFA ZA MIRADI MBALI MBALI
1.Ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Mtina mradi umeanza mwaka 2014 kwa ufadhili miradi ya benki ya dunia chini ya programu ya maji vijijini ( RWSSP- rural water services and sanitation program) .mradi unatekelezwa kwa jumla ya Tsh 455,545,277. Ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Mtina utahusisha ujenzi wa chanzo cha kisima chenye kutumia pump, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba ya kusambazia maji lenye urefu wa kilometa 10.8 na ujenzi wa vituo vya ksambazia maji 33, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 135,000.
Mradi huu bado unaendelea kutekelezwa, unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi June 2017. Jumla ya wakazi wapatao 7,680 wa vijiji vya Nyerere na Muungano watanufaika na mradi huu.
Picha
2.Ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Lukumbule, mradi ulianza mwaka wa fedha 2014 chini ya ufadhili wa benki ya dunia katika programu ya huduma ya maji vijijini (RWSSP). Mradi wa maji unatekelezwa kwa jumla ya Tsh 475,472,151. Ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Lukumbule utahusiha ujenzi wa chanzo ambacho kipi ndani ya ya eneo la kijiji cha lukumbule, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 135,000 (135m3), uchimbaji na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa 8.0 kilometa, ujenzi wa mfumo wa kuvuna maji ya mvua katika Shule ya Sekondari Lukumbule, Zahanati ya Lukumbule, Shule ya Msingi Mchesi, ujenzi wa fensi katika eneo la pump na ujenzi wa vituo 30 vya maji katika kijiji.
Mradi umekamilika na unafanya kazi. Jumla ya wakazi wapatao 6,437 wa vijiji vya Lukumbule na Mchesi wanapata huduma kupitia mradi huu.
Picha za kisima na taping place with community.
3.Ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Amani, chiungo /meamtwaro umenza mwaka 2014 chini ya ufadhili wa benki ya dunia kupitia program ya kuboresha maji vijijini (RWSSP), mradi unatekelezwa kwa jumla ya Tsh 1,039,776,320, Ujenzi wa miundombinu katika vijiji vya Amani, Chiungo/ Meamtwaro utahusisha ujenzi wa vituo 40 vya kusambazia maji ambavyo vitahudumia jumla ya wakazi wapatao 10,993 wa vijiji vya Amani, Chiungo, Meamtwaro na Mchengamoto, ukarabati wa matenki 2 yenye ujazo wa lita 50,000 katika kijiji cha Amani na Chiungo, ujenzi wa matenki 2 yenye ujazo wa lita 50,000 katika kijiji cha Chiungo na Amani, uchimbaji na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa klimeta 29.1 kutoka njia kuu
Mradi wa maji umekamilika na wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama.
Picha .
4.Ujenzi wa miundumbinu ya maji katika kijiji cha Matenganga umeanza mwaka 2014 chini ya ufadhili wa benki ya dunia katika programu ya kuboresha huduma za maji vijijini (RWSSP), mradi unatekelezwa kwa jumla ya 1,039,875,210. Ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha matemanga umeanza mwaka 2014. Ujenzi utahusisha ujenzi wa tenki 1 lenye ujazo wa lita 100,000 na ukarabati wa matenki 2 katika kijiji cha Matemanga na Jaribuni, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilometa 20.4, ujenzi wa chanzo cha kutumia pump, ujenzi wa vituo 36 vya kusambazia maji.
Jumla ya wakazi wapatao 7,727 wanakusudiwa kupata huduma ya maji baada ya mradi kukamilika na mradi upo katika hatua za utekelezaji bado.
Picha za visima na chanzo na taping area.
Ujenzi wa Miundombinu ya vyoo na madarasa katika shule ya Sekondari Nandembo, mradi umeanza mwaka 2015/2016 , ujenzi unatekelezwa chini ya mradi wa SEDEP II, utekezaji wa mradi huu ni ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ujenzi wa matundu 8 ya vyoo.
Ukarabati wa kisima cha Maji katika shule ya wasichana Masonya, ukarabati umefanywa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 imefanya ukarabati wa kisima hicho kwa kutumia tsh 2,000,000 ili kuhakikisha shule inapata huduma ya maji ya kutosha ili wanafunzi wapate muda wa kutosha kujisomea na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Ujenzi wa miundombinu ya Soko na Ghala la kuongeza thamani mazao ya Mpunga Nakayaya. Halmashauri kupitia MIVARF inatekeleza ujenzi wa Ghala na Soko la mpunga katika eneo la Nakayaya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, mradi unaotekelezwa ni wa mwaka wa fedha 2015/2016 wenye jumla ya tsh.833,845,470.00.
picha
Ukarabati wa Kisima cha Maji katika shule ya Sekondari Ligunga, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ilitenga tsh 2,000,000.00 kwa ajili ya kukarabati kisima cha maji katika shule ya sekondari Ligunga ili kupunguza tatizo la upatikanaji maji katika shule na kuberesha mazingira ya kusomea na kutolea elimu.
picha
Ujenzi wa daraja la Fundi Mbanga jimbo la Tunduru Kaskazini, mradi umetengewa jumla ya tsh 507,900.000.00 Road Fund 2015/2016.
picha.
Ujenzi wa Hosteli katika shule ya sekondari Matemanga-Tunduru kaskazini. katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 serikali ilitenga tsh 28,000,000.00 za ujenzi wa bweni ili kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.
picha.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.