• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Ziara Mkoani Ruvuma

Imewekwa : November 25th, 2017



Waziri Mkuu  Atoa Katazo la Wananchi Kuacha Tabia Ya Kukata Miti -Kalulu 

Akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha mbungulaji kilichopo kata ya Kalulu wilayani Tunduru, unaotekelezwa kwa mchango wa Halmashauri katika miradi ya maendeleo,wananchi pamoja na serikali kuu.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rahaleo baada ya kupokea  taarifa ya utekelezajiwa mradi wa uchimbaji wa visima viwili virefu katika kijiji cha Mbungulaji na Rahaleo waziri mkuu alisema serikali inatekeleza kwa vitendo sera ya ilani ya chama cha mapinduzi na imeanza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha kuwa kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama.

Na ili serikali iweze kufikia malengo hayo na kutunza vyanzo maji ni lazima wananchi kutunza mazingira na kuacha tabia ya kukata misitu ovyo kwani hali ukame maeneo mengi yanachangiwa na uharibifu wa uoto wa asili.

Waziri Mkuu akitoa maekelezo kwa wananchi na watumishi wa serikali wakati akiwa katika ziara mkoani Ruvuma, hapa ni katika kijiji cha Mbungulaji kata ya kalulu wilayani Tunduru.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliwataka wananachi kutunza mazingira na kucha tabia ya kufanya kilimo katika vyanzo vya maji na katika mabonde ambayo ni hifadhi ya maji

Vilele vile Mh. Majaliwa  alisema serikali imeweka fedha nyingi sana katika miradi ya maji katika kijiji cha mbungulaji na Rahaleo hivyo ni jukumu la wananchi kusimamia miundombinu hiyo ya maji na kuhakikisha kuwa baada ya mradi kukamilika unakuwa endelevu kwa kutunza mazingira yanayozunguka visima vya maji.

Alisema waziri mkuu “jumla ya  milioni 112 laki 226 mia 290 zimtengwa na serikali ya halmashauri kugharimia mradi huu hivyo ambapo katika kijiji cha mbungulaji shilingi milioni 28 laki 217 mia 660 zitatumika na katika kijiji cha rahaleo milioni 84 na elfu 9 mia 260 zitatumika”

Nimeelezwa kuwa mradi huu utawafikiwa wakazi  wapatao 4,879 ambapo kati ya hao Mbungulaji wakazi 1,799 na Rahaleo wakazi 3,080, na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika vijiji hivi kwani wananchi wanategemea visima vitatu tuu vinavyofanya kazi kwa sasa huku visima 15 miundombinu yake ikiwa imechakaa na visima vingine kukosa maji kutokana na kina cha maji kupungua, hali inayochangiwa na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili

kaimu Mkurugenzi Mtendaji wilaya Tunduru Ndg Chiza C Marando akisoma taarifa ya utekelezaji uchimbaji wa visima virefu vya maji katika kijiji cha Mbungulaji kwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa wakati akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kukagua ukamilifu wa barabara ya Lami inayoungana wilaya za Tunduru-Mangaka na Tunduru Namtumbo iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika kwa asilimia 100.

Viongozi wa vijiji vyote hakikisheni kuwa katika maeneo ya kuzunguka kisima miti ya kuhifadhi maji inapandwa mita 100  kuzunguka eneo hilo kila upande ili kulinda visima hivi visikauke na kukosa huduma ya maji alisema waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mhe.Kassimu Maliwa.

Aliendelea kusema kuwa serikali inatakeleza miradi mikubwa ya maji vijiji inayoendeshwa na serikali kwa ufadhili wa  benki ya dunia na Tunduru miradi hii inatekelezwa katika vijiji kumi, kuna mradi wa maji Lukumbule, Mtina,Matemanga, Mbesa, Amani ambayo ipo katika utekelezaji.

Waziri Mkuu wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. kassimu Majaliwa akisamia wananchi alipowasili katika kijiji cha Mbungulaji kata ya Kalulu wilayani Tunduru akitokea wilaya ya Namtumbo, kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera na Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme.

Waziri mkuu alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua wakandarasi ambao wanafanya miradi kwa kususua ikiwa ni pamoja na kuvunja mikata yao mara moja, hata hivyo alitoa muda wa wiki mbili kwa kampuni za wakandarasi wa maji katika mradi wa mtina na matemanga kukamilsha kazi ya ujenzi wa miradi hiyo kabla ya serikali kuwachukulia hatua.

Waziri mkuu Kassimu Majaliwa aliwaagiza viongozi wa wilaya kuwapa hao wakandarasi wiki mbili tu kama watakuwa hawajamaliza kazi kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kusitisha mikata yao mara moja.

Waziri Mkuu Mh.Majaliwa Kassimu Majaliwa akitoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya juu ya utunzaji wa mazingira kuzunguka vyanzo vya maji kwa kupanda miti mita mia kila upande kuzuia kukauka kwa vyanzo hivyo kutoka na mabadiliko ya tabia ya nchi.


Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.