Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imepokea jumla ya shilingi milioni 826 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari wilayani humo.
Shule zilizonufaika na fedha hizi ni pamoja na Shule ya Sekondari Nandembo, Shule ya Sekondari Tunduru, Shule ya Sekondari Masonya, Shule ya Sekondari Mataka, Shule ya Sekondari Matemanga, Shule ya Sekondari Tarajali Kata ya Mbati, Shule ya Sekondari Tarajali Kata ya Ngapa
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndg. Chiza C. Marando ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu ya elimu wilayani Tunduru. Amesema kuwa fedha hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari.
Ndg. Chiza C. Marando ametoa wito kwa wataalamu, wasimamizi wa mradi pamoja na wakandarasi waliopata zabuni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa ubora na kwa wakati. Pia, Amewaomba wananchi kusimamia miradi hiyo kwa karibu ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu ya elimu wilayani humo. Upatikanaji wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo bora utasaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu.
Halmashauri imeahidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi hii ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango vya juu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.