Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imeingiza kwenye mzunguko wa fedha zaidi ya bilioni 13.6 kupitia minada ya ufuta inayoendelea kufanyika katika wilaya ya Tunduru ,ambapo kufikia mnada wa nne uliofanyika katika kata ya mchesi Wilaya ya Tunduru imefanikiwa kufikia kuingiza katika mzunguko wa fedha takribani bilion 13.6 ," tumeingiza bilioni 13.6 katika minada minne ya ufuta" alisema meneja shughuli Chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD) Ndg . Marcelino mrope.
Aliyasema hayo katika mnada wa tano wa ufuta ulifanyika katika chama cha msingi NAMAKA (Namwinyu) , ambapo wakulima walikuwa na dhamana ya kuuza takribani tani 770 za ufuta ,ambapo wanunuzi nane (08) walijitokeza kununua ufuta huo, miongoni mwao wanunuzi wanne walifanikiwa kununua ufuta wote kwa bei ya shilingi 3,475.
Aidha afisa ushirika (W) Tunduru ndg. George Bisani aliendelea kuwasisitiza wakulima kutunza vipato vyao vizuri ili viweze kuwapatia maendeleo na kuyainua maisha yao , pia aliwataka vijana kuchangamkia fursa hii ya kilimo kwani kwa sasa kilimo ndicho kinachochangia katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa .
Pia aliendeleza kuvikumbusha vyama vya msingi kuzidi kuendelea kuwalipa wakulima kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.