Kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imepokea Zaidi ya bilioni 12 kwa ajili ya ruzuku ya walengwa pamoja na usimamizi ngazi ya wilaya.
Mratibu wa TASAF (W), Bwn.Muhidin Shaibu ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuonesha nia ya dhati katika kupambana na umaskini katika Wilaya ya Tunduru, ambapo Mpango huu wa kunusuru kaya maskini umejikita katika uhawilishaji wa ruzuku kwa walengwa, Miradi ya ajira za muda (PWP), Ruzuku ya uzalishaji, na Ujenzi wa miradi ya miundombinu.
“Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ina jumla ya kaya 20,228 kutoka katika vijiji 157 vilivyopo wilayani, Katika kipindi cha miaka mitatu ya awamu ya sita, tumefanya malipo kwa awamu kumi na tano” Alisema Bwn. Muhidin “Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa wilaya zinazolipa malipo kwa njia ya mtandao (e-payment) na Jumla ya kaya 4,341 zimepokea kwa njia ya Benki na kwa njia ya mtandao wa simu na kaya 15,887 zilipokea kwa mfumo wa fedha taslimu (cash)”
Vile vile, Halmashauri inatekeleza aina mbalimbali ya miradi ambayo ni uboreshaji visima vya asili, ujenzi wa barabara za jamii, mashamba ya miti na matunda, ujenzi wa vivuko na uchimbaji wa mabwawa ya kuhifadhi maji. Takwimu za miradi hii ni kama ifuatavyo, mikorosho idadi 36,257 katika eneo la ekari 323.7 imepandwa, miti ya mbao mitiki 36,790, ujenzi wa barabara za jamii km 1311, miti ya matunda miembe 560 eneo la ekari 14 na kuboresha visima 15 vya asili.
Kaya zote zilizoandikishwa kwenye Mpango ambazo hazina nguvu kazi zitapata ruzuku ya msingi,ruzuku ya kutimiza masharti ya elimu na afya. Kadhalika kaya zitapata fursa ya kuongeza kipato kwa kushiriki katika kazi za ajira ya muda.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa nchini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Lengo kuu la Mpango huu ni kuziwezesha kaya maskini zaidi kuweza kuongeza matumizi ili kumudu kugharamia mahitaji muhimu ya kaya.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.