Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa Halmashauri nchini ambayo imekuwa ikitekeleza sharia ya fedha ya kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayokusanywa kwa ajili ya kuwawezesha wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu waliopo kwenye makundi.
Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya 06, Halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo yenye Zaidi ya thamani ya Bilioni moja kwa vikundi 234, ambapo vikundi vya wanawake 95, vikundi vya Vijana 86, na vikundi vya wenye ulemavu 53.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii (W) Bi. Jecelyne Mganga, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kazi nzuri katika kuwafikia wananchi na kuboresha maisha yao, ikiwa ni pamoja kuwapatia mikopo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Amesema mikopo hiyo imewezesha makundi haya kuanzisha na kukuza biashara zao, na hivyo kuboresha maisha yao.
"Serikali ya awamu ya sita imeonyesha dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, Mikopo hii imekuwa msaada mkubwa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri yetu," amesema Bi. Jecelyne. "Uwezeshaji wa kiuchumi unawapa fursa ya kujikwamua kutoka katika umaskini na kujitegemea, Ninaomba wananchi wote waendelee kuunga mkono juhudi za Serikali hii ili tuweze kufikia malengo yetu ya maendeleo."
Pichani (Aliyevaa Miwani) ni Afisa Maendeleo ya Jamii (W), Bi. Jecelyne Mganga.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inaendelea kuipongeza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kazi nzuri wanayofanya. Wizara hii imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Sera za Serikali zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi. Pia Halmashauri inaipongeza Serikali kwa ujumla kwa dhamira yake ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.