Na theresia mallya Tunduru.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Juma Zuberi Homera wakati akizindua zoezi la ugawaji wa dawa za kingatiba kwa magonjwa yalikuwa hayapewi kipaumbele ngazi ya shule Wilaya iliyofanyika katika shule ya msingi Muungano.
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi mratibu wa chanjo wilaya kwa niaba ya Mganga mkuu wilaya Dkt.Wendy Robert alisema magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni pamoja na Kichocho, Minyoo ya Tumbo,Trachoma, Usubi, Mabusha na Matende, aliyataja magonjwa ambayo kingatiba hutolewa ngazi ya shule kuwa ni Kichocho na Minyooo ya tumbo.
Aidha alisema katika kipindi cha mwaka 2019 Halmashauri kupitia Idara ya afya kwa kushirikiana na Idara ya Elimu msingi wanatarajia kutoa chanjo kwa wanafunzi wapatao 71309 ikiwa wasichana 35288 na wavulana 36021 kutoka katika shule 150 za msingi wilayani Tunduru.
Mratibu wa chanjo alisema "Mwaka 2018 tulitarajia kutoa kingatiba kwa wanafunzi wapatao 67364 lakini wanafunzi waliokunywa dawa ni 65815 ikiwa Wasichana 32663 na wavulana 33152 sawa na asilimia 98 ya malengo tuliyotarajia kuyafikia ya asimilia 100 kwa wanafunzi wote wa shule za msingi wilayani Tunduru"
Magonjwa haya ya kichocho na minyoo ya tumbo huambikizwa kwa njia ya maji kwa binadamu mwenye vijimelea kutotumia choo hivoo vimelea kusambaa au kuchangamana na maji na huenea kwa binadamu kugusa maji hayo,huku minyoo ya tumbuo ikienezwa kwa u;aji wa vyakula visivyopikwa vizuri ama matunda yasiyooshwa vizuri, kutovaa viatu, kula bila ya kunawa mikono.
Katika picha ni wanafunzi wa shule ya msingi Muungano wilayani Tunduru wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa uzinduzi wa chanjo kinga dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele,ambapo jumla ya wanafunzi 71309 katika shule 150 wanatarajiwa kumeza dawa hizo kuanzia mei 03 2019.
Mratibu alisema kuwa madhara yatokanayo na magonjwa haya yasipotibiwa kichocho husababisha kutoka kwa damu kwenye mkojo na kinyesi,saratani ya tumbo, kibofu cha mkojo na ini.
Minyoo ya tumbo husababisha watoto kuwa dhaifu, kuishiwa damu, utumbo kujifunga na kifafa, mahudhurio hafifu na mandeleo duni shuleni.
Naye mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Juma Zuberi Homera alianza kwa kuwapongeza walimu wa shule ya msingi muungano kwa usimamizi bora katika taalum, pia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia idara ya afya kitengo cha uratibu wa chanjo kwa kufanya kazi ya usambazaji wa chanjo katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Tunduru.
Juma Homera aliwataka wazazi na walimu wote wenye watoto katika shule za msingi 150 wilaya ya Tunduru kuhakikisha watoto wote wanapata dawa za kinga dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele ili kuendandana na kauli mbiu ya ‘Tunduru bila magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele sasa inawezekana, timiza wajibu kwa kumeza dawa, kingatiba, ishi kwa furaha’
Watoto wapewe haki zao za msingi ikiwa pamoja na watoto kupewa haki ya kupata elimu katika mazingira rafiki kama upatikanaji wa chakula shuleni,hivyo niwaagize wazazi wote wa wilaya ya Tunduru tuwachangie watoto wetu chakula shuleni ili waweze kusoma vizuri na kutengeneza taifa lenye tija.
Nimalizie kwakuwaomba wazazi wote wilaya ya Tunduru kuhakikisha kwamba watoto wotewanakunywa dawa hizi ndani ya Wilaya ya Tunduru kwani hazina madhara yoyote kwaafya ila ni kinga dhidi ya magonjwa ya Kichocho,Trachoma,Minyoo ya tumbo, Mabusha,Usubina Matende.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.