“Tumeshuhudia katika vipindi tofauti katika nchi yetu wastaafu kupata mafao tofauti kutoka katika mifuko ya hifadhi ya jamii” alisema mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Zuberi Homera katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza na wafanyakazi kwa niaba ya mkuuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme , katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani (mei Mosi) ambayo kimkoa imefanyika wilayani Tunduru, Mh. Juma Homera alisema kauli mbiu ni kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi.
kuungunishwa kwa mifuko hii ya hifadhi ya jamii kunatarajiwa kuleta manufaa kwa wastaafu kwani watakuwa na uwezo mkubwa wa kumudu maisha baada ya kustaafu na kuwa na uhaikika wa kupata mahitaji yao muhimu na kupunguza idadi ya wategemezi.
Mtumishi hodari kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya Tunduru bi Neema Luvanda akikabidhiwa zawadi ya mfanyakazi Hodari na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh.Juma Homera katika maadhimisho ya sikukuu za mei mosi zilizofanyika kimkoa wilayani Tunduru katika viwanja vya CCM wilaya.
Pamoja na uboreshaji wa mafao ya wafanyakazi lakini pia mkuu wa wilaya alisema kuwa pamoja na sheria hii mpya kuanzishwa kuna mapungufu lakini serikali inaendelea kufanya maboresho na kutengeneza kanuni zitakazosimamia mfuko huu ili kuondoa tofauti zote na malalamiko ya wastaafu.
Aidha Juma Homera aliendelea kusisitiza masuala ya nidhamu,umoja na ushirikiano miongoni mwa watendaji katika kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi na kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa Umma bila ya ubaguzi wa itikadi za dini, siasa au kabila.
Hata alitoa maagizo kwa maafisa masuhuli kusimamia watendaji wanaosimamia ukusanyaji wa mapato kutotoa mwanya kwa baadhi ya wafanyabishara ambao wanakwepa kulipa kodi kwa vigezo mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.