Umefanyika muendelezo wa mafunzo ya uhifadhi rasilimali asili yaliyotolewa katika wilaya ya Tunduru kupitia uwezeshaji wa muungano wa mashirika ya uhifadhi wa rasilimali na maliasili .kwa Wilaya ya Tunduru ,shirika moja wapo la utoaji mafunzo hayo la Honeyguide limetoa mafunzo hayo kupitia mradi wa Kujenga Usimamizi Wa Asili (KUWA) wenye dhima kuu ya kujenga uwezo katika utawala wa kusimamia rasilimali na maliasili kwa usawa ili kutengeneza njia za kuboresha maisha na kuzalisha manufaa endelevu ya kiuchumi,kimazingira na kijamii.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na jumuiya mbili za uhifadhi wanyama pori za wilaya ya Tunduru ambazo ni NALIKA na CHINGOLI ambapo walipatiwa elimu juu ya utawala bora na jamii endelevu zenye mahusiano chanya na uhifadhi wa rasilimali na maliasili na mazingira kwa ujumla.
Afisa mjenga uwezo wa shirika la Honeyguide ndg.Prosper Frank Munisi amewataka wananchi wa jumuiya hizo za uhifadhi kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali zetu ,mafunzo haya waliopata wanajumuiya ya uhifadhi wa rasilimali yatawasaidia katika kuwa na uwezo wa kusimamia rasilimali hasa katika misingi mitatu ya uendelevu wa kijamii,uendelevu wa kiuchumi na uendelevu wa kimazingira kwa usawa.
Pia alisema anawaomba wanajumuiya za uhifadhi kushirikiana katika kutatua changamoto zinazokumba uhifadhi wa rasilimali na maliasili katika meneo yetu tunayotoka.
Mfunzo hayo yalihudhuriwa pia na mwenyekiti wa jumuiya ya NALIKA wilaya ya Tunduru pia ni mwenyekiti wa muungano wa jumuiya za uhifadhi Tanzania ,Ndg.Saidi Rashidi Masoud , kwa upande wake aliwataka wanajumuiya wote ,elimu hiyo waliopata waweze kuinenza kwa wananchi wa maeneo waliotoka ili nao waweze kuwa na elimu juu ya uhifadhi wa rasilimali za asili na kuweza kupunguza uvamizi na ujangili ambavyo ni vitendo vitakavyoweza kupoteza maliasili na rasilimali zetu.
Tunaushukuru muungano wa mashirika ya uhifadhi wa rasilimali na maliasili hasa Honeyguide kwa mafunzo haya tuliyoyapata tunahaidi kuyatendea kazi yale yote tuliyoyapata kwa manufaa ya uhifadhi wa mazingira na maliasili alisema miss Jamila Abdallah, askari uhifadhi wanyamapori (VGS) kijiji cha twendembele.
Baadhi ya wanajumuiya za uhifadhi wa rasilimali na maliasili wilaya ya Tunduru wakiwa katika kundi la majidiliano,wakijadili kuhusu visababishi vya uharibifu wa maliasili na rasilimali asili katika maeneo yetu.wanajuiya wakiwa katika darasa kujifunza kuhusiana na utawala bora na jamii endelevu katika kuhifadhi rasilimali na mali asili ili kuleta tija katika misingi ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.