Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na rasilimali za vyakula vya Mifugo Dkt.Asimwe Lovince Rwiguza wakati wa kukabidhi mbegu za nyasi aina ya Rhodes kwa uongozi wa halmashauri baada ya kusikia kilio cha wafugaji wengi kukosa malisho katika vitalu walipangiwa na halmashauri hasa wakati wa kiangazi.
Akitoa pongezi kwa kazi kubwa iliyofanywa na halmashauri kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alisema serikali imeona jitihada zilizofanywa katika kuhakikisha kuwa wafugaji wanapata maeneo ya malisho ya kudumu, hali ambayo ipunguza na kuondoa migogoro iliyokuwepo ndani ya wilaya yenu.
Wafugaji na viongozi kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi wakipanda shamba la mfano katika kijiji cha Masonya
Serikali kwa kutambua mchango huo imeamua kuleta mbegu za nyasi za kisasa ili kuondoa tatizo la malisho. "tumeanza kwa kuleta kilogramu 65 za nyasi aina ya Rhodes ambazo zitapandwa katika vitalu vya wafugaji ambao wamepangiwa maeneo na halmashauri lakini pia mbegu nyingine zitaendelea kuletwa ili kuondoa tatizo la malisho"
Aidha Dkt. Asimwe alipongeza halmashauri ya Tunduru kwa kutekeleza maagizo ya viongozi kwa vitendo kwani ndio halmashauri pekee nchini ilitenga maeneo, kuwapanga wafugaji na kufanya taratibu za umilikishaji.
Hata hivyo alitoa rai kwa wakurugenzi nchini kujifunza namna halmashauri ya Tunduru ilivyotekeleza kwa vitendo zoezi la kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji, pia aliwataka wafugaji kuchukua mbegu hizo na kupanda katika msimu wa vuli.
Na kwa upande wake mwakili wa wafugaji Mzee Rugwasha Mtwegambuli aliishukuru serikali ya halmashauri kwa kuwatengea maeneo ya kufugia, na pia kutambuliwa na serikali kwani awali kabla ya kupewa vitalu waliishi kwa manyanyaso sana.
Alisema "tunampongeza sana rais John Magufuli kwani tunaona kazi anazofanya na anatujali sana, tunaishukuru pia halmashauri kwa kutupatia maeneo ya malisho na tunafuga kwa nafasi na hakuna migogoro tena kwa wakulima na wafugaji"
Akitoa shukrani kwa wizara mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Homera aliishukuru wizara kwa kuona juhudi zinazofanywa lakini pia alisema bado kuna changamoto katika maeneo ambayo wamepelekwa wafugaji kwani hakuna mito ya maji karibu hivyo serikali ione namna yaa kuwezesha upatikanaji wa maji ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza kwa wafugaji kusafiri umbali mrefu kutafuta hasa wakati wa kiangazi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.