Wakulima wilaya ya Tunduru wamezidi kuneemeka kwa kuona mafanikio ya mfumo wa uuzaji mazao kwa njia ya stakabadhi ghalani ,kwa zao la ufuta baada ya kufanyika minada miwili katika wilaya ya Tunduru na kufanya shilingi bilioni 6.4 wameingiziwa wakulima baada ya kufikia kuuza zaidi ya tani 1600.
Ambapo katika mnada wa kwanza waliuza ufuta tani 857 kwa bei ya sh. 3,822/= , na mnada wa pili kuuza zaidi ya tani 769 kwa bei ya shilingi 3,895/=
Wakulima wameendelea kuishukuru serikali chini ya mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mfumo huu wa kuuza mazao stakabadhi ghalani. Na kukishukuru na kukipongeza chama kikuu cha ushirika Tunduru (TAMCU LTD) kwa kusimamia mfumo huo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.