Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Mhe. Julius Mtatiro amewataka wakulima wa zao la korosho kutumia vizuri fedha wanazopata katika kuwapeleka watoto shule na kukata bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa ili kusaidia familia katika kuleta maendeleo wilayani Tunduru.
Ameyasema hayo katika mnada wa tatu wa Korosho uliofanyika katika kijiji cha majimaji tarehe 21 Novemba 2019 ambapo kampuni mbili za Alfa Choice na Sunshine zilishinda zabuni hiyo kati ya wanunuzi 34 waliojitokeza katika mnada huo ambapo jumla ya kilo 2,979,407 zilinunuliwa kwa bei ya wastani ya shilingi 2773.19 kwa kilo.
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika wilayani Tunduru Ndg.Hashimu Mbalabala akitoa matokeo ya Mnada wa tatu kwa wananchi wa Majimaji waliojitokeza kushuhudia mnada huo kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Tunduru ambapo wanunuzi walikua 34 lakini waliotenda kwa bei ya juu na kununua korosho zilizokua mnadani ni Kampuni ya Sunshine na Alfa choice kwa bei ya shilingi 2773.19 kwa kilo.
Aidha Mhe.Mtatiro amewapongeza wanunuzi walioshinda zabuni hiyo na kuwataka wanunuzi wanaotenda kwa bei ya chini kuwa hawatapata Korosho za wilaya ya Tunduru hivyo wajipange.
Pia mkuu huyo wa wilaya ametoa maagizo kwa mkuu wa jeshi la polisi wilayani Tunduru kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko ya wanunuzi wa korosho ya kukumbana na vipingamizi barabarani wanapowahi katika minada ya kununua korosho Tunduru. “OCD fanya mawasiliano na wenzio wa wilaya jirani ili kuondoa usumbufu kwa wanunuzi wanapawahi kwenye mnada Tunduru” alisema Julius Mtatiro.
Vile vile aliwata mweneyekiti wa chama kikuu cha Ushirika pamoja na Meneja wa Chama hicho kuhakikisha kuwa magunia kwa ajili ya kufungashia korosho za wakulima yanafika kwa wakati wilayani Tunduru ili kuhakikisha korosho zilizopo katika maghala ya vijiji zinasasfirishwa kwenye ghala kuu kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Afisa Ushirika Wilaya Ndg.George Bisani akisoma barua za zabuni za wanunuzi wa zao la Korosho katika mnada wa tatu uliofanyika katika Kata ya Majimaji.
Hata hivyo alimalizia hotuba yake kwa kuwaagiza viongozi wa bodi ya korosho kuandaa mkutano na vyama vyote vya msingi wilayani Tunduru ili kuondoa sintofahamu inayoendelea kwa baadhi ya vyama na waandhishi wanaowaibia wananchi, na wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na ununuzi haramu wa korosho (Kangomba) ili serikali iwachukulie hatua kwani kufanya hivyo ni kumkandamiza mkulima.
Theresia Mallya
Tunduru
22/11/2019
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.