• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

WAKULIMA mbaazi waingiza bilioni 9 Tunduru.

Imewekwa : September 14th, 2023

Wakulima Wilayani Tunduru wameingiza Zaidi ya bilioni 9 baada ya kuuza Mbaazi tani 4,732 katika minada minne iliyofanyika kwa msimu huu wa mwaka 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Mkuu TAMCU LTD ndg. Imani Kalembo, katika mnada wa nne uliofanyika katika kijiji cha Mkanyageni AMCOS ya Nakatete Wilayani Tunduru Septemba 14, 2023, amewahamasisha wakulima kuendelea kulima zao la Mbaazi kwa wingi kwa kuwa pamoja na kuwa ni zao la chakula lakini hivi karibuni limekua zao la biashara.  

“Tunduru tuna bahati kubwa sana kwasababu tunalima mazao yanayofuatana kwa msimu, kwa hiyo mwaka mzima mkulima anakua ananufaika kwa kupata fedha kwa ajili ya maendeleo yake”. Alisema.

Pichani: Meneja Mkuu wa TAMCU ndg. Imani Kalembo (Mwenye kipaza sauti)

Aidha, katika Mnada wa nne kampuni 11 zilijitokeza kushiriki katika mnada huo, kampuni tatu zilifanikiwa kuingia katika ushindani ambapo zilifikia wastani wa bei ya kununua mbaazi kwa wakulima, ambapo tani 700 ziliuzwa kwa bei ya shilingi 2,015 kwa kilo moja.

Wakulima wameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mfumo wa Stakabadhi ghalani, ambao umeonekana kuwa na tija kwa mkulima.

Pichani: Wakulima wa kijiji cha Mkanyageni wilayani Tunduru.

“Tulikua tunalima na kuuza mbaazi kwa bei ya chini sana kabla ya kuwepo mfumo wa stakabadhi ghalani, mfumo huu umekua ni mkombozi ukilinganisha na walanguzi waliokuwa wakinunua kwa bei ya kutupwa”. Hayo yalisemwa na Bi. Shakira Kazembe Bakari, Mkulima wa Mbaazi toka kijiji cha Mkanyageni.

Mnada huo ulihudhuriwa na wakulima wengi wa mbaazi huku wakionyesha furaha yao kwa bei ya juu iliyopatikana kwenye mnada huo ambayo iliongezeka ikilinganishwa na mnada wa tatu ambapo wakulima waliuza mbaazi kwa shilingi 1,948.

Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.