Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Denis Masanja, ameshiriki sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba kwa mwaka 2025 yaliyofanyika tarehe 28 Agosti 2025 katika uwanja wa Shule ya Msingi Msinji, Kata ya Ligoma, Tarafa ya Namasakata, Wilaya ya Tunduru.

Mafunzo hayo yalihusisha vijana 175 (wanaume 150 na wanawake 25) ambao walianza mafunzo rasmi kuanzia tarehe 03 Aprili 2025. Hata hivyo, kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ugonjwa, utoro na utovu wa nidhamu, ni wahitimu 78 (wanaume 69 na wanawake 9) pekee waliomaliza mafunzo hayo kwa mafanikio.
Kwa kipindi cha miezi mitano (sawa na wiki 21), vijana hao wamefundishwa kwa nadharia na vitendo masomo mbalimbali yaliyotolewa na JWTZ pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, sambamba na mihadhara ya viongozi wa taasisi za serikali na binafsi.
Malengo makubwa ya mafunzo hayo ni kuwajenga vijana kuwa wakakamavu, wazalendo na walinzi wa kwanza katika vijiji, kata na mitaa yao, ili kushirikiana na vyombo rasmi vya ulinzi na usalama kulinda amani ya nchi.
Mafunzo ya Jeshi la Akiba ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha wananchi wanajengewa uwezo wa kushiriki katika kulinda amani, usalama na mshikamano wa kitaifa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.