"Waandishi wa Habari watakiwa kuwa wakala wa mabadiliko katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa wazazi kusimamia watoto kujua K tatu" hayo yamesemwa na Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma Profesa Riziki Shemdoe katika kikao kazi cha mrejesho wa simulizi za mabadiliko kilichofanyika katika ukumbi wa Jimbo Mbinga.
Akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa washiriki kutoka katika Halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma na waandishi wa habari, Afisa mipngo mkoa ndg Edmund Siame alisema lengo la mrejesho wa simulizi za mabadiliko ni kubadilishana na kujifunza mbinu walizotumia kufanikiwa katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya elimu mkoani kupitia mpango wa Tusome pamoja.
washiriki wa Tusome Pamoja wakimsikiliza katibu Tawala Mkoa Profesa Riziki Shemdoe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa Simulizi za mabadiliko kutoka katika Halmashauri zote nane za mkoa wa Ruvuma.
Alisema ili kuleta uhalisia na kutoa mrejesho chanya kwa wafadhili wa huu wa Tusome Pamoja ni Halmashauri zote kutoa simulizi zenye uhalisia kwa kuzingatia chazo tatizo, ukubwa, takwimu halisi zinazohusiana na tatizo hilo na suluhisho.
"natoa agizo kwa Afisa Habari Ofisi ya mkuu wa mkoa kushirikiana kwa karibu na maafisa walioko katika Halmashauri zote nane kuwajengea uwezo wa kuandaa makala za simulizi za mabadiliko kuonesha ufanisi wa kazi zinazofanywa katika Halmashauri zao na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla"
Afisa Mipango Ndg. Edmund Siame alisema kuwa ili kutokomeza tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuesabu katika mkoa wa Ruvuma linaweza kuisha kwa kushirikiana vizuri na waandishi wa habari kwani ni wakala wa amabadiliko katika jamii wakitumiwa vizuri.
Mratibu wa Mpango wa Tusome Pamoja mkoa wa Ruvuma ndg Stephen Msabaha akiongea na washiriki kutoka halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma (ambao hawako kwenye picha) wakati wa Ufunguzi wa mkutano siku mbili wa kutoa mrejesho wa maandalizi ya Simulizi za Mabadiliko
"niwaombe waandishi wa habari kutoa na kutengeneza vipindi vya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu kwa wazazi pamoja na walezi kusoma na watoto wao jioni wanaporudi nyumbani lakini pia kuwa na tabia ya kufuatilia na kukagua madaftari ya watoto ili kujenga ueuelewa,ajua vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko " alisema Kaimu katibu Tawala mkoa ndugu Edmund Siame
vilevile alisema mpango wa Tusome Pamoja wamefanya kazi kubwa toka umeanza ikiwa ni utoaji wa vitabu vya kusoma darasa la kwanza na pili, kuboresha madarasa na matundu ya vyoo pamoja na mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Muwezeshaji wa Mpango wa Tusome Pamoja Taifa Ndg Furaha Kabuye akitoa maoni ya maboresho ya Simulizi za Mabadiliko zilizokuwa zinatolewa na washiriki kutoka Halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma.
"Mapitio yafanyike kwa wanafunzi wa darasa la pili wanaoingia darasa la tatu wasijua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu wachujwe na kurudishwa darasa la pili ili kumaliza kabisa tatizo KKK katika wa Ruvuma ifikapo 2020 , na niwaagize Maafisa Elimu wote kufanya mapitio ya wanafunzi waliopo sekondari wasiojua KKK kuondolewa mara moja"
Hata hivyo aliwapongeza washiriki kwa kazi kubwa waliofanya kwani inatia moyo kuona kuna mabadiliko chanya yanayochangiwa na Kamati za shule, wahamasishaji Elimu Jamii (WJE), Umoja wa wazazi na walimu (UWAWA), wadau mbalimbali wa Elimu na Halmashauri zote kutoa ushirikiano mkubwa kuchangia mpango wa Tusome Pamoja katika kuboresha Miundombinu ya madarasa, Upatikanaji wa chakula shuleni na kupunguza wanafunzi wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.