Katika hatua ya kuhakikisha kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linafanyika kwa ufanisi na kwa uwazi, viongozi wa vyama vya siasa nchini wamefanyiwa mafunzo maalumu. Kiongozi wa Mafunzo hayo akiwa ni Afisa Mwandikishaji Jimbo la Tunduru Kusini na Kaskazini Ndg. Chiza C. Marando.
Mafunzo haya yamelenga kuwapa viongozi hao uelewa wa kina kuhusu mchakato mzima wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa daftari sahihi katika uchaguzi huru na wa haki. Viongozi hao wametakiwa kuhamasisha na kutoa elimu sahihi kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao.
"Mafunzo haya ni muhimu sana kwani viongozi wa vyama vya siasa wana nafasi kubwa ya kuhamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha. Alisema Ndg. Marando “Tunatarajia kuwa baada ya mafunzo haya, viongozi wetu wataweza kutoa elimu sahihi na kuondoa misingi yote ya shaka."
Mafunzo haya ni muhimu sana kwani yanawawezesha viongozi wa vyama vya siasa kuwa mabalozi wazuri wa zoezi hili kwa wananchi, ili kuhakikisha kuwa daftari la kudumu linaakisi hali halisi ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.