Leo tarehe 25/11/2022 umefanyika uzinduzi wa siku kumi na sita za kupinga ukatili kwa akina mama na watoto katika wilaya ya tunduru uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha kajima kata ya jakika.
Katika uzinduzi huo mwenyekiti msaidizi wa Halamshauri ya wilaya ya Tunduru alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo na kauli mbiu ya siku kumi na sita za upingaji ukatili kwa kina mama na watoto ilikua
“KILA UHAI UNA THAMANI TOKOMEZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO”
Kampeni hii ya kupinga ukatili na kuimalisha harakati za upatikaji wa haki za binadamu ambayo inaanza Novemba 25 hadi 10 December ambazo ni siku kumi na sita za kupinga ukatili wa wanawake na watoto.
Katika siku hizo kumi na sita (16) za kupinga ukatili zidi ya wanawake na watoto inaambatana na sikukuu za kimataifa ambapo tarehe 29 November ni siku ya ya watetezi wa haki kwa wanawake, December 1 ni siku ya ukimwi duniani na tarehe 10 december ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu.
“KILA UHAI UNA THAMANI TOKOMEZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO”
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.