Miradi ya ukarabati wa majengo ya vituo vitatu vya afya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru umekamilika kwa asilimia 95. halmashauri ilipokea shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kukarabati wa vituo vitatu vya afya vya mkalase milioni 400, Mchoteka shilingi milioni 400 na kituo cha afya Matemanga milioni 500 ambazo zimetumika katika ujenzi wa majengo matano katika kila kituo cha afya.
Ukarabati na upanuzi wa vituo hivi vitatu vya afya ndani ya wilaya ya Tunduru vitaboresha utoaji wa huduma za afya kwani wilaya hii ina eneo kubwa la kiutawala ambalo linahitaji uboreshaji wa huduma za afya na miundombinu ya kutolea huduma hizo, ili kupunguza changamoto za wananchi kusafiri umbali mrefu kutata huduma za afya.
Halamshauri hii ya Tunduru ina hospitali tatu moja ikiwa ni ya serikali na 2 zinamilikiwa na taasisi za dini, na vituo vitano vya afya ambavyo huduma zake zilikua duni kwani zilikosa baadhi ya majengo kama ya upasuaji mdogo, jengo la mama na mtoto, maabara, wodi pamoja na nyumba za waganga hivyo kutoa huduma hafifu.
katika picha ni muonekano wa majengo ya kituo cha afya Matemanga kilichopo wilaya ya Tunduru jimbo la Tunduru kaskazini ikiwa ni mojawapo ya vituo vitatu vya afya vinajengwa na serikali ya awamu ya tano katika utekelezaji wa utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi na kuhakikisha kuwa serikali inafika katika uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Vituo hivi vya Mkasale na Mchoteka vilivyopo katika Jimbo la Tunduru Kusini na Kituo cha Afya Matemanga kilichopo Jimbo la Tunduru kaskazini kukamilika kwake na kuwepo kwa wataalam wa kutosha kutapunguza sana tatizo la kinana mama kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kiwango kikubwa ndani ya wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.