Katika mafunzo hayo leo wajumbe walipata kujifunza juu ya muimili muhimu wa fedha katika jumuiya hizi za uhifadhi wa maliasili na rasilimali zetu, katika mafunzo hayo kulizungumziwa suala muhimu la kuongeza mapato ya ndani ya jumuiya za uhifadhi ambapo afisa mjenga uwezo wa WMA alitaja vyanzo muhimu vya mapato vitakvyokuwa tija kwa jumuiya za uhifadhi maliasili kwa uendelevu wa kiuchumi kwa jumuiya na jamii kwa ujumla ambavyo ni Hewa ya ukaa, Utalii wa picha na Utalii wa uwindaji.
Mjenga uwezo alisema biashara ya hewa ukaa kama chanzo cha mapato kwa jumuiya za uhifadhi inaweza kuingiza zaidi ya milioni 400 kwa mwaka ,aidha alitaka jumuiya za uhifadhi kuzidi kutunza na kuhifadhi misitu ili biashara hii iwe na tija kubwa kwa jumuiya za uhifadhi kwa ushirikiano na jamii zinazotuzunguka kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Aidha kaimu afisa maliasili na uhifadhi wa mazingira (W) Ndg.Dunia Almasi kwa upande wake aliliomba shirika la Honeyguide kuwa na uratibu wa mafunzo hayo kwa viongozi wa vijiji ,madiwani na hata maafisa tarafa pia elimu hii iweze kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa lengo kubwa la kujenga uelewa kwa wananchi. “uhifadhi utakuwa na tija zaidi kama utagusa ngazi ya kaya moja moja” alisema.pia afisa maliasili alitoa changamoto kubwa inayoikumba sekta ya uhifadhi maliasili kwa wilaya ya Tunduru ya ukosefu wa wawekezaji na kuwaomba wawekezaji kuja kuwekeza katika uhifadhi wilaya ya Tunduru kwa maslahi mapana ya wanajamii.
Kwa upande mwingine afisa maendeleo ya jamii Bi Jeseline Mganga alisema katika jumuiya hizi tuna jukumu la kuhamasisha katika uanzishwaji wa vikundi kwa ajili ya kutunza pesa na kujipatia mikopo itakayo wasaidia katika kuanzisha shughuli nyingine za kuwaingizia kipato zitakazowasiaidia katika kujikwamua kiuchumi .
Mafunzo ya takribani siku nne(04) juu ya uhifadhi wa rasilimali na mali asili za nchi yetu yanayotolewa na muungano wa jumuiya za uhifadhi wa wanyama pori Tanzania (CMWA) ,leo June 11, 2023 yametamatishwa katika wilaya ya Tunduru ,mafunzo hayo yakiwa yalilenga kutoa elimu juu ya uhifadhi wa rasiliamli na maliasili ambapo kwa wilaya ya Tunduru yalitolewa na shirika moja wapo la uhifadhi mali asili lijulikalo kama Honeyguide .
WAJUMBE WA MAFUNZO YA UHIFADHI WA MALIASILI NA RASILI,ALI WAKIWA KATIKA ZOEZI LA KUKUMBUSHANA YALE WALIOPATIWA NA WAWEZESHAJI WA MAFUNZO HAYO (katikati ni ndg Selemani (mkufunzi) ).
#tembo na maendeleo
#misiti ni pesa
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.