Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imeanza utekelezaji wa zoezi la uhakiki wa kaya zilizojenga na kuboresha vyoo kwa mwaka 2022/2023
Zoezi hilo limeendeshwa na kusimamiwa kikamilifu na Afisa afya wilaya ya Tunduru Ndg. Ayubu Majumbewima akishirikiana na wajumbe waliopangiwa kwa eneo husika.
Majumbewima alisema, vyoo bora na salama ni muhimu kwa afya na ustawi wetu. Uboreshaji wa vyoo unaweza kuwa na athari kubwa katika kuzuia magonjwa na kuboresha maisha ya jamii nzima.
Ambapo kata nne za wilaya ya Tunduru zimefanikiwa kupitiwa na zoezi hilo la uhakiki ambazo ni kata ya Majengo, Nanjoka, Mlingoti Mashariki na Nakayaya.
Pia zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji ilani kwa wale wote ambao hawakutekeleza agizo la uboreshaji huo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.