Milioni 259 Zaboresha Elimu –Nandembo Sekondari
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika mwaka wa fedha 2016/2017 imetekeleza miradi mingi katika sekta ya elimu na Shule ya Sekondari Nandembo ni miongoni mwa shule nchini zilizopata mradi mkubwa P4R wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, hosteli 2, ujenzi wa matundu 10 ya choo na ukarabati wa maabara tatu za masomo ya sayansi.
Mradi huu ulianza kutekelezwa katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2016/2017, umetekelezwa kwa mafanikio makubwa kwani hadi kufika sasa umekamilika kwa asilimia 90.
jengo la maabara ya masomo ya sayansi katika shule ya sekondari nandembo iliyokabatiwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia mradi wa P4R.
Katika ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vimekamilika kwa asilimia mia na vinatoa huduma kwa wanafunzi hivyo kupunguza usumbufu kwa wanafunzi na kuondoa mlundikano wa wanafunzi katika madarasa.
Vilevile kwa upande wa ujezi wa hosteli mbili ujenzi upo katika hatua za umaliziaji na hivyo hosteli hizo zitaanza kutumika mara baada ya kukamilika.
haya ni matundu ya vyoo vya kisasa ambayo yamekamilika na yanatumika kwa sasa
“hosteli hizi zitaongeza tija kwa wanafunzi kuishi katika mazingira ya shule, kupata muda mwingi wa kujisomea, kuishi mazingira salama hasa wanafunzi wasichana na kuthibiti nidhamu ya wanafunzi wetu”alisema mkuu wa shule ya nandembo mwalimu Marry Ndunguru
Pia ujenzi wa matundu kumi ya choo unaendelea na ukarabati wa maabara tatu za masomo ya sayansi umekamilika kwa asilimia 90.
“kukamilika kwa ujenzi wa maabara kutaongeza tija kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi kwa sababu watakuwa wanafanya mazoezi kwa vitendo tofauti na ilivyokuwa hapo”
Mkuu wa shule ya sekondari Nandembo aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na dkt. John Pombe Magufuli kwa kuipa sekta ya elimu kipaumbelekwa kuwapekelea mradi wa P4R kwani umetatua changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa, hosteli pamoja na matundu ya vyoo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.