Wilaya ya Tunduru ni moja ya wilaya zenye wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF).
Kupitia mratibu wa TASAF wilaya ya Tunduru Ndg Muhidini Shaibu akizungumzia mpango huo ambao unalipa awamu ya pili ya malipo ya mwezi wa tano (5) na mwezi wa sita(6), mpango huo wa kunusuru kaya maskini unahudumia kaya takribani 12,740 katika vijiji 88 na jumla ya pesa zinazolipwa kwa kaya zote ni jumla ya TZS 484,362,000. Na malipo haya yatafanyika ndani ya siku tisa.
Pia mratibu wa TASAF alitoa wito kwa walengwa wa mpango huo kutoa taarifa zilizo sahihi ili kuondoa changamoto ambazo huwa zinajitokeza wakati wa malipo ya ruzuku zao.
Pia aliwahamasisha walengwa kuunda vikundi vya ujasiriamali ili hizo pesa wanazofaidika nazo ziweze kuwasaidia katika matumizi yao ya kila siku ,pia aliwasihi walengwa waweze kuwapeleka watoto wao shule kama mpango unavyosema na kuwapeleka watoto wao wao wachanga kuhudhuria kiliniki ili kuweza kuendeleza afya iliyo njema kwa watoto wao.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.