• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TUSESCO YAKABIDHI SETI 45 ZA MEZA NA VITI TUNDURU SEKONDARI

Imewekwa : February 25th, 2022

Tusesco ni Umoja wa Waitimu katika Shule ya Sekondari  Tunduru ambao waliitimu miaka ya 1985 adi 1990 ambapo Mwenyekiti  wa Tusesko Bw.John  Maongezi  amesema “Jumuiya ya Tusesko tangu ianzishwe kupitia Wanachama wake inachangishana fedha kwa lengo la kutatua matatizo mbalimabali yanayo ikabili shule hiyo ya Tunduru sekondari  ambapo kabla ya kuandaa meza na seti za  viti walichukua mawazo ya Walimu ili kuangalia kipi ni kipao mbele cha shule kwa sasa ndipo jibu likapatikana kuwa kuna upungufu wa seti za  Meza na  viti  kwaiyo  jumuiya ikaona ni vizuri kuchonga seti za Meza na viti 45”.

Aidha Tusesco kupitia Mwenyekiti  wake imesema nia ya kuendelea kuichangia  Tunduru sekondari bado wanayo  na malengo ya kuhakikisha shule yao ya Tunduru sekondari inaendelea kuwa na miundombinu na Taaluma bora bado wanayo  sababu vipaumbele bado wanavyo pia kutoa hamasa kwa wanafunzi  ambao wanaoendelea kusoma na waliomaliza katika shule hiyo wawe na moyo wa Uzalendo wa kuipenda shule yao.

Kwa Upande wake Mkuu wa Shule Tunduru Sekondari Bw.Namlya Ismaili amesema “Nawashukuru sana Waitimu waliomaliza tangu shule inaanzishwa adi miaka ya 1990 kwa wao kujitoa kwa Uzalendo wao wakuonyesha nia ya kuiunga mkono  serikali kwa kuipatia Tunduru Sekondari  seti za meza na viti 45 vyenye gharama ya Shilingi Milioni tatu laki sita na ishirini elf ( Tzs.3,620,000/=) uku akihaidi kuwa watatunza Vitu vyote vya shule ikiwemo na misaada mbalimbali wanayo patiwa na wadau wa maendeleo kama hao Waitimu wa zamani katika Shule hiyo”.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Julius Mtatiro kwa upande wake baada ya kupokea  msaada huo wa seti za meza na viti kutoka kwa Waitimu hao wa zamani katika Shule ya Sekondari Tunduru amesema “Walichokifanya Tusesco ni kuunga mkono jitiada zinazofanywa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuhakikisha kuwa miundombinu ya kusomea Wanafunzi wetu inakuwa bora ikiwemo kupata hizo seti 45 za meza na viti ambazo Tusesko wametoa katika shule yao pendwa waliosoma tangu inaanzishwa adi miaka ya 1990” pia Mkuu wa wilaya ya Tunduru amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw.Sostenes Bwilo kuwa iandaliwe Cheti maalum ambayo itakuwa na majina ya Watu wote wa TUSESCO ambao ni Wanafunzi wa zamani wa Tunduru sekondari kwa Uzalendo wao wamejitolea  seti 45 ya meza na viti  kwahiyo cheti hicho kitasainiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Pia Kaimu Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bw. Sostenes Bwilo wakati akimkabidhi Mkuu wa shule ya Sekondari Tunduru  Bw.Namlya  Ismaili seti 45 ya meza na viti amemtaka kutunza vizuri mali hizo za shule ili ata kipindi kijacho walioisaidia shule hiyo watakapo fika tena wazikute mali za shule zipo salama lengo waendelee kuwa na moyo wakuisaidia zaidi shule hiyo ya Tunduru Sekondari.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • HARAMBEE YA UJENZI WA OFISI YA CCM TUNDURU YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 106 PAMOJA NA MIFUKO 15 YA SARUJI.

    December 29, 2025
  • MHESHIMIWA SEFU HASSAN DAUDA NDIYE MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU

    December 05, 2025
  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.